Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,956
- 5,330
Uhakiki wa wajumbe hao unafanyika kwa kuita majina ya wajumbe wa kanda mojamoja ili kupata uhalali wa wapigakura wanaotambulika ndani ya katiba ya chama hicho, ambao wataamua kati ya Freeman Mbowe, Tundu Lissu, na Charles Odero nani apewe kijiti kuiongoza Chadema.
Mbowe anatetea nafasi hiyo aliyoiongoza kwa miaka 21, anachuana vikali na Makamu wake bara, Tundu Lissu. Uchaguzi huu unafanyika leo, Jumanne, Januari 21, 2025, katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Agenda hiyo imetangazwa na Katibu Mkuu Chadema, John Mnyika. Uchaguzi huu unasimamiwa na wazee wanane wastaafu wa Chadema, ambao ni Profesa Raymond Mushi (Mwenyekiti), na Katibu akiwa Dk Azaveli Lwaitama. Wengine ni Ruth Mollel, Ahmed Rashid, Alfred Kinyondo, na Azumuli Kasupa.