Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,776
Mwanzoni mwa mwaka huu katika kusherehekea kutimiza kwangu miaka 20 tangu nizaliwe, nilipata zawadi ya mkoba kutoka katika viwanda vya hapa kwetu. Mkoba ni nadhifu sana, bidhaa za ngozi huwa zinadumu kwa muda mrefu. Kasoro kubwa ilikua kwenye kumalizia, hadhi ya zipu hailingani na ubora ya mkoba.
Kama nilivyosema awali bidhaa za ngozi ni imara sana. Kuipa heshima bidhaa ya ngozi zipu na vifungo ni lazima viwe kwenye ubora unaondana na thamani ya bidhaa.
Ni vigumu kubuni mtindo wa pochi na ukubalike na wengi sokoni. Watengenezaji wwngi wanaiga mitindo ya wabunifu wakubwa kama Yve Saint Laurent (YSL), Gucci, Channel na baadae wakina Kelvin Claine ba DKNY wanatoa toleo kwa bei nafuu zaidi.
Wabunifu wetu wawe wanafuatilia matoleo ya wabunifu wakubwa ili kuvutia soko. Zipu zianaweza kuagizwa kutoka Uturuki au China, mradi ziwe zenye ubora. Unaweza kuweka kichwa cha zipu chenye logo ya kampuni. Hapa hata mshona viatu hawezi kuiga.
Hali kadhalika kwa mikanda ya kiume na ya kike. Pamoja na makubazi ya kike na ya kiume.