Ubungo: Wanawake 36 wanaodai kukamatwa na kudhalilishwa kuwa "Dada Poa" kumfikisha mahakamani DC Hassan Bomboko na kumdai Fidia ya Tsh. Bilioni 36!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
93,081
162,316
Wanawake 36 wa Ubungo waliokamatwa na Mkuu wa wilaya hiyo wakidaiwa Kuwa ni makahaba na kuwekwa lupango siku 5 sasa watamfikisha mahakamani Mkuu huyo wa Wilaya

Wakili Madeleka amesema Wateja wake 36 watamdai Mkuu wa Wilaya ya Ubungo fidia ya TSH 36 billion Kwa kuwadhalilisha

Ameandika Wakili Msomi Madeleka ukurasani X

Hii June ina mambo Sana 😂


Watuhumiwa wanaodaiwa kufanya biashara ya kuuza miili yao (dada poa) waliokamatwa na Mkuu wa wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam Hassan Bomboko, kupitia mawakili wao wakiongozwa na Wakili Peter Michael Madeleka, wametuma barua kwa Bomboko wakidai fidia ya Tsh. bilioni 36.

Kupitia barua hiyo wakili Madeleka ameeleza kuwa madai ya fidia hiyo yanakuja kufuatia udhalilishaji waliofanyiwa wateja wao sambamba na kuwekwa rumande pasipo sababu za msingi, ambapo amesema wateja wao wameagiza kulipwa fidia hiyo ndani ya siku 14.

Imeelezwa kuwa kuanzia Juni 14 na 15 mwaka huu, Mkuu wa wilaya huyo alitumia madaraka yake vibaya kwa kuwaita watuhumiwa hao (dada poa) na kudai kuwa wamekuwa wakijihusisha na biashara ya ukahaba kwenye eneo la Tip Top -Manzese, ambapo aliongoza oparesheni ya kuwakamata wadaiwa hao kutoka kwenye vyumba vyao na kuwapeleka kituo cha Polisi Mburahati ambako wamesota huko kwa takribani siku 5.

Barua hiyo imeendelea kufafanua kuwa ndani ya kipindi hicho Bomboko aliendelea kuagiza Jeshi la Polisi kutotoa dhamana kwa watuhumiwa hao jambo ambalo ni kinyume na katiba na halikubaliki kwenye taswira ya sheria na ulinzi wa ‘Haki za Binadamu’, sambamba na hilo kufuatia maelekezo yake Juni 18 na 19 mwaka huu wateja wao walipelekwa kwenye Mahakama ya Hakimu mkazi Sokoine Drive, Dar es Salaam lakini hakuna mashtaka yoyote yaliyosomwa dhidi yao.

Amesema malipo ya fidia wanayodai inatokana na hasara ya kiuchumi waliyosababishiwa, madhara yasiyo ya kiuchumi, maumivu na mateso, msongo wa mawazo, maumivu ya kihisia, kupoteza furaha ya kuishi, kushuka kwa sifa na hadhi nzuri kwa jamii waliyoitengeneza kwa muda mrefu, na kwamba malipo ya fidia hiyo yafanyike papo hapo na endapo itakuwa tofauti hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
1718896538173.jpeg

Pia soma
- Mkuu wa Wilaya ya Ubungo adhamiria kutokomeza biashara ya ukahaba

- Vita ya DC Ubungo na Makahaba: Mgongano wa sheria, haki na maadili

- Tetesi: - Waliokamatwa kwa tuhuma za kununua Makahaba Ubungo kumburuza mahakamani Mkuu wa Wilaya kwa kudhalilishwa! Wadai walifuatwa Guest!

- Kuna kesi ya udhalilishaji kama wale walioonekana kwenye video ya kukamata makahaba watapata mwanasheria mzuri

- Vigezo gani anavitumia DC wa wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko kuvamia kumbi za starehe na nyumba za wageni kukamata watu anaodai ni makahaba?
 
Mkuu wa wilaya mjinga kabisa kuwahi kutokea,mahakamani kuna kesi za msingi zinahitaji kusikilizwa,wewe unakamata watu kwa jambo la kijinga ambalo linapelekea shida kwenye mahakama zetu.

Tuna matatizo mengi sana tofauti na huo ukahaba anaopambana nao, wacha wamuadabishe,huko aliko najua hana hamu.

Bado najiuliza wanasheria wa halmashauri zetu wana kazi gani juu ya kuwaongoza hawa watu kipi wafanye na kipi wasifanye?, au ni ubabe wa wateule kuwa wao ni kila kitu na mwisho wa siku wanaangukia pua?.

Mimi na ualimu wangu huu wa grade A najua kabisa hapa nikiingia kichwa kichwa lazima mambo yanigeukie,vipi kwa mkuu wawilaya ambaye ana wataalamu wa kila aina wakuweza kumshauri?
 
Wanawake 36 wa Ubungo waliokamatwa na Mkuu wa wilaya hiyo wakidaiwa Kuwa ni makahaba na kuwekwa lupango siku 5 sasa watamfikisha mahakamani Mkuu huyo wa Wilaya

Wakili Madeleka amesema Wateja wake 36 watamdai Mkuu wa Wilaya ya Ubungo fidia ya TSH 36 billion Kwa kuwadhalilisha

Ameandika Wakili Msomi Madeleka ukurasani X

Hii June ina mambo Sana 😂
anatumbuliwa Very soon
 
Mimi nilipomuona mke wa Madeleka, nikajua hiyo familia ya Madeleka ina matatizo makubwa. Mke na mume wote mitambo, na yote imefukuzwa kazi serikalini.

Kama unq kesi yako serious usimpe Madeleka, vinginevyo uwe na Hakimu au Jaji ambaye ni robot. Watoa maamuzi ni binadamu, anaweza kuwakoroga kwa ukichaa wake, wakabonyeza ki-uzi chembamba ukajikuta unakosa haki au unaipata kwa kuteseka sana.

Be wise when choosing an advocate. The best advocate is the one who does not wish to lose the court
 
Mkuu wa wilaya mjinga kabisa kuwahi kutokea,mahakamani kuna kesi za msingi zinahitaji kusikilizwa,wewe unakamata watu kwa jambo la kijinga ambalo linapelekea shida kwenye mahakama zetu.

Tuna matatizo mengi sana tofauti na huo ukahaba anaopambana nao, wacha wamuadabishe,huko aliko najua hana hamu.
Kosa lake ni kukamata watu walikuwa lodge
 
Mimi nilipomuona mke wa Madeleka, nikajua hiyo familia ya Madeleka ina matatizo makubwa. Mke na mume wote mitambo, na yote imefukuzwa kazi serikalini
Acha uongo waliacha kazi wenyewe, jamaa anatembelea V8 ya kwake na anaenda popote duniani kwa hela ake, jiulize ni OCD gani anaweza kuruka Tanzania nzima kwa pesa ake na nje ya nchi?
 
Hatuna sheria kukataza kujiuza.

Hata kama ingekuepo (kuna nchi ipo) ugumu huja kwenye kuthibitisha kweli huyu mtu anajiuza.

Mavazi ambayo mdada anavaa kutembea barabarani ni hayo hayo mdada mwingine anavaa kujiuza.

So kwa Tz hua anakamatwa na kesi huishia wilayani kwa kulipa faini 50K kwakua hatuna ushahidi zaidi ya kumkuta kasimama na hatuna sheria inayokataza.

Nahisi kwa sasa Tz tunapromote sana 50/ 50 DC ana mtihani hapa. But anashtakiwa yeye au serikali?
 
Back
Top Bottom