Ubinafsishwaji Bandari tatizo la Watanzania ni lugha ya Kingereza, Mkataba upo sawa

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,873
11,121
ELimu, Elimu, Elimu ni kitu muhimu sana. Tanzania tuna tatizo kubwa ya lugha ya Kingereza kwa watu wetu. Lugha ya Kiswahili haina maneno na misamiati iliyojitosheleza, hivyo tafsiri toka Kingereza kwenda Kiswahili mara nyingi kumejaa ukanjanja na uwongo.

Tatizo kubwa kubwa ni watu kutafsiri Kingereza kwenye lugha zao mama, halafu baadae kutafasiri kwenda Kiswahili!

Article 23 kati ya Mkataba wa Emirates of Dubai na Serikali ya Tanzania kuhusu usimamiaji na uendeshaji wa bandari unapotoshwa hapa JF.

Article 23 inazungumzia Termination and Duration, hakuna sehemu yeyote inayosema serikali ya Tanzania au Emirates of Dubai hawaruhusiwi kuvunja mkataba. Mkataba utaweza kuvunjwa kwa makubaliano ya pande zote mbili, ndio kilichoandikwa.

Artcle 20 inazungumzia dispute settlement, Mkataba unazungumzia ikitokea kuna kutokuelewana kwenye article 23 basi usuluhishi ufuate Sheria za Kimataifa na mazungumzo yafanywe kwa Kingereza, yafanyike Johanesburg Afrika ya Kusini kwa pande zote kuwa na wawakilishi.

Tuache kupotosha raia kwa mihemko ya kisiasa na wengine kufikia hatua ya kumtukana Rais, tatizo sio Mkataba tatizo ni watu kutokuelewa lugha ya Kingereza.
 
Ukiwa unajua Watanzania elimu ni tabularasa kwa nini usiwatafsirie wakauelewa kabla hamjaujadili?

Nchi hii ni ya viongozi wanaozungumza kiingereza au ya wananchi?

Nilizaliwa uswahilini usinilazimishe niwaze kizungu.
 
Kwahiyo waTanzania wote ni mazuzu ila nyie wachumia tumbo wachache ndo wenye Akili sana ya kuchambua Mikataba ya Kiingereza siyo?

Msituone wajinga sana, ifikie mahali tuheshimiane na Kama ni Keki ya Hili Taifa wote tuifaidi Huku tukiandaa na Keki ya Vizazi vijavyo navyo waikute Tanzania Bora.
 
Hakuna ata hiyo mikataba, as yet. Hiyo ni framework tu. Ata hiyo agreement inataka HGA zikisainiwa ziwe siri.

Mambo wanayopigia kelele Article 20 na 23; ni mambo ya kawaida if anything ni aspects za ‘stabilisation clauses’ ata sijui kwanini wameziweka tofauti.

Na hakuna mkataba wa kimataifa popote duniani usio na ivyo vipengele. Nimeskiliza Lissu contract
law inaonekana is not his thing, maelezo yake yana upotoshaji mkubwa. Sio kwa makusudi, ila uelewa.
 
tena tunakwambia wewe mtoa uzi kama umelipwa uje ueneze ujinga wako hapa umejidanganya. Na unajisifia umesoma elimu yako inamsaada gan. Wenzio wameuza hvo v2 na wanauhakika wa maisha wataspend the rest of their lives ila wew 2tabk wote bongo hapa hapa tnalialia na hapo ndo utajua kua mchicha unaota ila haukoromi
 
Mkataba uvunjwe kwa makubaliano ya pande mbili …kwa hiyo anae under perform au asietekeleza wajibu wake halafu akakataa hayo " Makubalino ya pande mbili ' nini kinatokea ?

tunataka TOR za Mkataba sio blaa blaaa
Mkuu umewahi fanya biashara kweli wewe?

Unawezaji kuvunja mkataba bila makubaliano
 
Unajua maana ya iyo article 23?, Kwenye mikataba kinaitwa Umbrella clause ambayo ukiiangalia vizuri inamlinda zaidi mwekezaji kuliko sisi na ndio wanakitumia huko kote walikowekeza kunyonya na Incase ikatokea mgogoro hiyo article 20 haiwezi kusaidia ukizingatia wanasheria wa serikali ya CCM kushinda kesi nje ni nadra kwanza wanakula mlungula tu kwaiyo tunaweza kujikuta watanganyika tumeangukia kwenye madeni yasiyo na kichwa Wala miguuView attachment 2649684
 

Attachments

  • 20230607_172556.jpg
    20230607_172556.jpg
    51.8 KB · Views: 9
Kwenye hili itoshe kuonyesha kuwa kama nchi tuna matatizo moja kwenye uongozi bora na pili elimu.

Haiwezekani taifa lenye 60+m kushindwa kuwa na watu wenye uwezo wa kuendesha bandari mpk tuanze leo kutoleana maneno, kama tatizo ni kuunderperform kwa bandari tulipaswa kufanya utafiti kujua shida ni nini zikishabainika na kwa kuwa bandari ni eneo ambalo lina mapato ya kutosha ni serikali kuamua kufanya uwekezaji mkubwa pale maana uhakika wa return ya uwekezaji ipo ila hii ya kuona kila kushindwa ni kutafuta uwekezaji hapana mbona Tanesco miaka nenda rudi ni shida haijatafutiwa mwekezaji?

Shida ya pili ni elimu serikali hii inataka kutuaminisha kuwa elimu yetu ni tatizo imeshindwa kutupa watu competent kuendesha mambo yetu.

Kwenye hili la bandari serikali imetupa nguo imeamua kutembea uchi wa mnyama.
 
Back
Top Bottom