Uanzishwaji wa "High Schools" za Masomo ya Sayansi Kwenye Sekondari Zetu za Kata: Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,524
1,173
Tumeanza kupata usajili wa "High Schools za Masomo ya Sayansi:"

(i) Suguti Sekondari itakuwa na "High School" ya masomo ya: PCM, PCB, CBG na EGM

(ii) Mugango Sekondari itakuwa na "High School" ya masomo ya: CBG na EGM

Kila Sekondari iliyotajwa hapo juu ina maabara 3 za masomo ya sayansi, bweni moja au mawili. Maji na umeme vipo.

(iii) Kasoma Sekondari ni shule kongwe yenye "High School" ya masomo ya: HKL, HGK, HGL na imeongezewa HGFa na HGLe

Umuhimu wa kuwa na "High Schools za Masomo ya Sayansi:"

Vijana wa Tanzania, wakiwemo wa Musoma Vijijini wanapaswa watayarishwe kuingia kwenye ushindani wa Ulimwengu wa sasa na ujao, yaani ushindani wa AJIRA, TAALUMA, UBUNIFU, UCHUMI, n.k.

Maoteo (global forecast) ifikapo Mwaka 2030:

(i) Utakuwepo upungufu wa wataalamu Milioni 80 ifikapo mwishoni mwa Mwaka 2030

(ii) Makampuni makubwa Duniani yatatumia takribani USD 3.2 Trillion kwa kila mwaka kuwekeza kwenye Artificial Intelligence (AI) ili kutatua tatizo la ukosefu wa wafanyakazi Duniani (growing global labour shortage). Roboti zitatumika kwa wingi!

High Schools zaidi za Masomo ya Sayansi zinahitajika Jimboni mwetu:

Sekondari zifuatazo ziendelee kukamilisha mahitaji ya uanzishwaji wa "High Schools" za Sayansi:
(i) Bugwema (wana maabara 3)
(ii) Nyakatende (maabara 3)
(iii) Kiriba (maabara 3)
(iv) Etaro (maabara 2 + computer room)
(v) Rusoli (maabara 2)
(vi) Makojo (maabara 2)
(vii) Nyambono (maabara 2)

Maombi ya michango ya ujenzi wa maabara:

Wanavijiji wanaendelea kuomba WADAU wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa Musoma Vijijini waanze na waendelee kushirikiana na SERIKALI kuchangia ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye Sekondari zetu za Kata.

Picha iliyoambatanishwa hapa inaonesha wanafunzi wa sekondari wa Jimboni mwetu wakiwa kwenye somo la vitendo la kemia (chemistry practical class).

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatano, 3.7.2024

WhatsApp Image 2024-07-03 at 17.06.59.jpeg
 
Back
Top Bottom