Nyarupala
JF-Expert Member
- Jun 2, 2024
- 466
- 826
Tanzania imepokea ndege kutoka Jeshi la Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambayo imetolewa kwa ajili ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mapokezi hayo yameshuhudiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, viongozi wa serikali na jeshi pamoja na Balozi wa Tanzania katika Falme za Kiarabu, Luteni Jenerali Mstaafu, Yacoub Mohamed.
Waziri Tax ameeleza kuwa ndege hiyo ni sehemu ya msaada wa jeshi la UAE ambao uliambatana na mafunzo kwa marubani wa Jeshi la Tanzania.
#HabarileoUPDATES