U-kocha ni kazi ngumu, kisa kidogo...

MtotoKautaka

JF-Expert Member
Jul 16, 2018
327
845
Ilikuwa mwaka 2022 nilienda kigoma kutembea kidogo.
Kigoma maeneo ya manyovu huko, baada ya kama wiki hivi nikawa nishazoeana na wadau hasa wapenda mpira.

Nilikuwa naenda mara Kwa mara kutizama mazoezi na kucheza siku moja moja.

Siku moja ile timu nilokuwa napiga nayo mazoezi wakapata ki mechi dhidi ya Kijiji jirani.
Wale jamaa wakanichagua mimi niwe kocha wao, sikupinga nikakubali.
Kumbuka it's real watu wa kigoma ni wabishi, hawaogopi hovyo na kukubadilikia ni sekunde.

Kikosi tulipanga pamoja ila wao ndo walipanga kwa asilimia zaid ya 90.
Mechi ikaanza baada ya kama dk 30 tukapigwa chuma, kwahyo tukawa nyuma kwa goli moja.

Nimekazana kuwaelekeza nini wafanye kwasabab ukiwa nje unaona vizur kuliko aliyeko ndani kwahyo nikawa nawaelekeza elekeza.

Kipindi cha kwanza mwishoni tukaongezwa la pili Kwa mpira wa Kona na kichwa.
Tukaenda half time tumenyongea watu wanafokeana tu kwa kutokufanya jinsi walivyopaswa kufanya.

Kipindi cha pili kinaanza tumefanya mabadiliko mawili beki wa kati na kiungo namba kumi.
Dakika za mwanzoni tu tukawa tunaona striker kama anatukaba badala ya kufunga.

Sasa niliposimama nimezungukwa na mashabiki kibao wengine wanasema hilo li jamaa (striker) litoe halijui chochote. Mimi pia nikawa nimeona kabisa ule mchezo haukuwa wa yule jamaa maana alikuwa hafanyi chochote zaid ya kuzunguka tu uwanjani.

Tukawa tumejiandaa kumfanyia sub tunasubir tu mpira utoke.
All over sudden yule jamaa kapewa pasi kapiga chenga kafunga, eh watu wote wakaruka kwa furaha jamaa noma jamaa noma jamaa anajua jamaa anajua, kelele za hajui zilipotelea kusiko julikana.

Kumbuka tayari tushamuinua mtu na anayetakiwa kutoka ni yule jamaa alofunga goli, sasa nikawa namwambia jamaa wa sub ajiandae ebana wale jamaa mashabiki acha wanibadilikie "hatoki, huyo jamaa hatoki tena toa mwingine siyo huyo mwamba anajua lilikuwa swala la muda"

Eh nikajisemea sasa hawa jamaa dk sifuri tu wameshanibadilikia, dk kumi hazijapita jamaa kaongeza la pili, aseee watu walimbeba yule mwamba wakimshangilia Kwa furaha sana.

Game ikaendelea mashabiki wakawa hawataki kabisa kusikia jamaa eti nataka kumfanyia sub na yule alikuwa anatakiwa kuingia majamaa wakamwambia atafute namba nyingine ya kucheza kama anataka kucheza na siyo kumtoa yule mshikaji.

All in all ile game tulishinda bao 3 Kwa 2, liliongezwa bao jengine dk za mwishoni kabisa, ila yule striker hakutoka na alishangiliwa sana wakati na baada ya mechi.
 
IMG-20241208-WA0098.jpg
 
Back
Top Bottom