GREAT VISIONAIRE
JF-Expert Member
- Sep 28, 2012
- 365
- 453
Mpambano uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu wa uzito wa juu duniani kati ya Tyson Fury vs Anthony Joshua umeenda mlama baada ya bondia Deontay wilder kutumia nguvu ya mkataba kutaka pambano la tatu sawa sawa na mkataba.
Pambano hilo litafanyika Tarehe 24 Julai na wengi wanaamini kuwa Deontay Wilder atakalia kidole tena kutoka kwa bondia bingwa wa uzito wa juu mbwatukaji Tyson Fury.
Mpaka sasa wanaosenaTyson Fury atashinda ni wengi zaidi sababu wanazozitoa:
1: Muda ambao Deontay Wilder ametumia kujiandaa ni mdogo kulinganisha na Tyson Fury ambaye amekuwa akijiandaa kwa muda mrefu kwa pambano la mchumba Anthony Joshua.
2: Tyson Fury amekuwa akijiandaa kwa muda mrefu na ameongeza uzito kufikia pauni 300 sawa na 150kg
Trainer wa Mayweather promotions Jeff Mayweather ameonyesha kumkubali Deontay Wilder japo anasema katika huu mpambano Tyson Fury ana asilimia kubwa ya kushinda.
Pia tukiangalia katika Historia za ndondi, ubingwa huwa ni era(muda). Ukishakutupa mkono mida basi, rejea Tyson ambaye alikuwa prime toka 1985 na alitembeza kichapo kwa muda wa miaka 10mfululizo kabla hajawa tyson bonge nyanya.
Floyd Mayweather amekua mjanja kwa kuliona hilo na aliamua kukaa chini mapema.
Umri wa Tyson Fury ni miaka 32 na Deontay wilder ni 35 yrs.
Karata yangu nampa Deontay wilder