Watu wanaingia kwenye madawa kutokana na sababu mbalimbali kama:-
1. Makundi rika
2. Kupoteza au kupunguza stress
3. Kuhisi ni fasheni au ujanja kula ngada
4. Kutafta stimu kali baada ya mtu kuwa sugu kwa vilevi vingine
5. Kukata tamaa
6. Kushawishiwa na mpenzi
7. Kuanzishiwa yani kuchanganyiwa kwenye sigara au bangi. Ila sababu kubwa ni ulimbukeni
Kuacha unga ni ngumu sana sababu ni mtamu sana, stimu yake ni very unique. ila kuacha pia inategemea uko steji gani kama unauvuta, unasnifu au unajidunga.
Pia maumivu ya arosto ni makali sana.
Nb kasi ya unga kuenea ni kubwa saana hasa ktk maeneo ya mijini na pia unapatikana kirahisi sana!!
Makundi ambao yako hatarini sana kula unga ni wanafunzi, wanaofanya shughuli zao maeneo ya stand, malaya, wasanii na wacheza mpira