Tuzo za TMA zitathaminika pale tu wanasiasa mtakapoacha kuziingilia

Mr Why

JF-Expert Member
Nov 27, 2019
1,732
3,313
Tuzo za TMA zimejaa aibu kubwa sana, uendeshaji wake unawashangaza hata waanzilishaji wa Tuzo Duniani. Tuzo za sanaa huwa zinadhaminiwa na watu wanaohusika na sanaa tu na sii vinginevyo.

Grammy Awards, BET Awards, Oscar Awards hazina mahusiano na Serikali ya Marekani bali support kubwa inatoka kwenye kiwanda cha sanaa peke yake ndiyo maana wakurugenzi wa tuzo hizo ni wale wasanii wastaafu pamoja na management nzima ya sanaa ya Marekani.

Sio hivyo tu hata waendeshaji wa shughuli nzima ya utowaji wa tuzo wanakuwa wametoka ndani ya kiwanda cha sanaa.

Ninyi TMA msiokuwa hata na jicho la aibu mmeingiza siasa ndani ya tuzo zenu mara vyama vya siasa mara sijui viongozi wa nchi aibu kubwa hii, pia siku ya utoaji wa tuzo viti vya mbele wanakaa viongozi wa siasa badala wakae wasanii wastaafu na wakurugenzi wa kiwanda cha sanaa cha Tanzania.

Bila aibu watoaji wa tuzo hizo wanowakabizi wasanii tuzo ni wanasiasa hawaishii hapo tu wanataja mpaka majina ya viongozi wa nchi badala ya wakurugenzi wa sanaa.

Tuzo za sanaa ni uwanja wa wasanii wa kujimwaga wao ninyi wanasiasa waachieni wasanii uwanja wao acheni kuwaingilia na kuwakosesha uhuru wao.

Tuzo za sanaa ni kipande kidogo sana kwahiyo msiingize serikali kwasababu mnaishushia serikali hadhi yake mwisho wa siku inaonekana ina deal na vitu vidogo.

Ndio maana Diamond Platnumz anaona aibu kwenda kwasababu tayari mmeshapoteza ile maana ya tuzo za wasanii hivi mnadhani kwa kasoro hizi hata mkiwaalika wasanii wa nje kama Davido, Burna Boy watakuja? Jiulizeni hili swali acheni kasoro hizi nchi nyingine zitawacheka kila siku, hii ni aibu kubwa sana.

Mnataka kukua na kupandisha hadhi ya hizi tuzo je kwa kasoro hizi mtathaminika?
 
Back
Top Bottom