Tuzo za Muziki Nchini: Maoni ya Wadau juu ya nini kifanyike ili kuongeza Tija, Mvuto na Kupunguza Malalamiko

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
677
1,098
1683549201037.png

Mnamo Aprili 29 kuamkia April 30 mwaka 2023 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakishirikiana na Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo waliandaa tuzo rasmi kwa ajili ya kuwapongeza wanamuziki wa Tanzania (Tanzania Music Awards). Baadhi ya walifanikiwa kunyakua tuzo hizo kwenye vipengele mbalimbali; Soma: Wasanii walioshinda Tuzo za Tanzania Music Awards 2023.

Pamoja na ugawaji wa tuzo hizo kumeibuka mitazamo na malalamiko kadhaa kuhusu utaratibu unaotumika katika zoezi zima la kupendekeza wawaniaji tuzo na washindi wa tuzo zenyewe.

JamiiForums kama miongoni mwa mdau wa muziki imeandaa mjadala wa kwenye Twitter Spaces ili kuwapa fursa watu mbalimbali kutoa maoni ya nini kifanyike ili kuongeza tija, mvuto na kupunguza malalamiko katika tuzo hizo.

Ili kutoa maoni yako tafadhali jiunge kwenye Twitter Spaces ya Jamiiforums siku ya Alhamisi ya tarehe
11 Mei 2023 kuanzia Saa: 11 Jioni - Saa 2 Usiku.

Pia unaweza kuandika maoni yako kwenye uzi huu, ambayo yatasomwa siku ya mjadala.

== Updates ==
- Mjadala umeanza, Taji Liundi ataongoza mjadala huu.

1683818215570.png


Maoni ya Master J (Mtayarishaji wa Muziki)
1683817752195.png

MASTER J (Mtayarishaji wa Muziki): Ninavyokumbuka Tuzo ilianza miaka ya 1999, ilifanyika Hotel ya White Sand, kipindi hicho, James Dandu ndio alikuwa muasisi wa wazo hilo.

Baadaye zinawa zinasimamiwa na Kampuni ya Bia, ilikuwa inatupa motisha ya kufanya kazi kwa umakini na nzuri kwa kuwa kazi zetu zilikuwa sikitambulika.

MASTER J (Mtayarishaji wa Muziki): Baadaye tuzo zikaanza kupoteza sifa hadi ikafikia hatua zikafungiwa, lakini kabla ilikuwa ni kitu kizuri sana, ilikuwa hata unapofikia kuingia kwenye Tano Bora ilikuwa ni heshima kubwa sana.

Ilipoanza kupoteza sifa na hatimaye kufungwa, sasa hivi ndio tunaona #BASATA wanapambana kuirudisha japo imerejea ikiwa na mambo mengi.

MASTER J: Ila sidhani kama Tuzo zimekufa, kuna changamoto ndogondogo tu ambazo najua zikifanyiwa kazi zinaweza kurejesha hadhi yake kama ilivyokuwa zamani.

Mfano suala la kumwambia msanii aombe wanatakiwa kuiondoa, nimefanya utafiti, moja wapo ni Tuzo ya American Music Association hawana kitu kama hicho, sijui huu utaratibu wameutoa wapi, mimi nimekuwa nikiupinga siku zote na haya ninapofanya mahojiano nimekuwa nikizungumza hilo.

MASTER J: Kipindi cha nyuma hakukuwa na changamoto ya kupata wasanii wanaotakiwa kufika kwenye Hatua ya Tano bora, hakukuwa na changamoto hiyo kabisa

Kamati ambayo ilikuwa inaundwa kipindi kile ilikuwa na mjumuisho wa watu ambao wanaujua muziki na walikuwa kwenye kiwanda cha muziki, wanaujua na hata ingetokea unawaamsha usiku wa manane au muda wowote wangekwambia nini kinaendelea.

MASTER J: Tatizo kubwa lilianza ambapo memba wa kuandaa wanachukua rushwa, na hilo ndilo ambalo lilifanya tuzo zipoteze sifa kuanzia hapo.

Maoni ya Wakazi (Msanii wa Hip Hop)
1683816985380.png

WAKAZI (Msanii): Tangu mwanzo Tuzo zimekuwa za BASATA, imekuwa ikisemwa kuwa wazo lilikuwa ni la Dandu pekee lakini kulikuwa na mtu mwingine nyuma.

BASATA walikuwepo pia na hata utayarishaji ulipohamia kwenye Kampuni ya Bia walikuwepo.

Kuhusu tuhuma za rushwa kama alivyosema Master J, nadhani kilichofanyika kulikuwa na watu wanaochezesha mfumo wakati wa mfumo wa kupiga kura kwa njia ya SMS

Pia kulitokea utimu ambao ulichangia Tuzo zianze kupoteza mwelekeo, hiyo ilichangia wapiga kura ambao wakati mwingine walikuwa ni wananchi wa kawaida walikuwa wanampigia kura mtu ambaye unakuta hana vigezo vya kushinda.

Kuna Wasanii wadogo wanafanya kazi nzuri lakini kw akuwa hawana majina ndio maana tunaishia kuwapa tuzo wasanii wenye majina

Snoop Dog hana tuzo za Grammy lakini Eminem na Jay Z wana tuzo kibao, hiyo inamaanisha unaweza kuwa mkali na usipate Tuzo

Lakini sisi tunataka kuwapa Tuzo wasanii wakubwa ili wasinune.

BASATA hawakutaka mtu mwingine aanzishe tuzo, alipojitokeza yeyote kuanzisha waliweka masharti kuwa wasiweke vipengele ambavyo vinaendana na Tuzo zao, wakasababisha watu washindwe kuanzisha Tuzo kwa masharti yao hayo.

Tuzo zimerudi tumependa ni jambo zuri lakini kuna mambo ambayo yamekuwa mapengo, ni bora siziwepo kwa kuwa zinaonekana hazina thamani.

Mfano watu ambao hawajatuma kazi zao hamuwapi heshima kisha mnaishia kuwapa heshima wale wengine ambao wanaoziponda tuzo.

Kipindi kile ilifikia hatua Wema Sepetu anasema mpigieni kura mtu fulani, Watu walikuwa wanamfuata anavyozungumza na wanampigia kura Mtu ambaye hastahili.

Kulikuwa na Utaratibu wa mafunzo kwa Wasanii wakieleweshwa kuhusu Tuzo mwezi mmoja kabla kisha wanapata posho, siku hizi wanaitwa siku moja kabla ya utoaji Tuzo Sioni haja ya kuwa wasanii wakituma ionekane wamejidhalilisha sana, ni kwa sababu Tuzo zinaonekana hazina thamani ndio maana inaonekana si sawa kwa Wasanii kutuma kazi

Maoni ya Mrisho Mrisho (Mratibu wa Tuzo za Muziki Tanzania kutoka BASATA)
1683817600975.png

Mrisho Mrisho (Mratibu wa Tuzo za Muziki Tanzania kutoka BASATA): Hizi ni tuzo za mahiri na si tuzo za umaarufu, lengo ni kutuza wasanii waliofanya kazi bora zaidi.

Kabla ya Tuzo tilikuwa na shughuli za kufanya, kwanza ni tathimini ya Tuzo za 2021, pili tulitengeneza Kamati ambayo ilitengeneza muongozo wa Tuzo za 2022

Kamati walipewa kazi ya kufanya utafiti na kushauri Serikali nini cha kufanya, baada ya hapo tukaingia kwenye Tuzo zenyewe.

Muitikio ulikuwa mkubwa, Wasanii walijitokeza kuleta kazi zao, baada ya hapo ikafuata ratiba ya uthibitisho kwa siku kadhaa

Baada ya kupembua zikabaki kazi zilizoingia kwenye Akademi, wakipembua kazi 1,109 hadi zikabaki 227, kisha Majaji tukawapa 60% na Wananchi ni 40%.

Muitikio ulikuwa mkubwa, Wasanii walijitokeza kuleta kazi zao, baada ya hapo ikafuata ratiba ya uthibitisho kwa siku kadhaa

Baada ya kupembua zikabaki kazi zilizoingia kwenye Akademi iliyoundwa na wajumbe kutoka Bara na Visiwani, wakipembua kazi ambazo idadi yake ilikuwa 1,109 hadi zikabaki 227, kisha Majaji tukawapa 60% na Wananchi ni 40%.

Kazi ya Akademi haikuwa kazi ya wazi japo tuliwaonesha lakini hatukuweza kuweka wazi wanafanya nini hasa. Mwenyekiti wa Majaji alikuwa John Kitime, na walipewa siku 5 ya kufanya kazi yao kuanzia asubuhi hadi jioni.

Ili Msanii apate tuzo anatakiwa kupata kura kutoka pande zote (majaji na jamii).

Kuna kipengele cha Muziki wa Reggae kwa Wanawake akidi haikutimia, walipatikana wasanii wawili na ilikuwa wanatakiwa kuwa angalau watatu, hivyo waliitwa na kupewa cheti vya kuthamini kazi zao

BASATA hatukuwa na kazi ya kuingilia majukumu ya majaji, tuliwaacha majaji wafanye kazi zao.

Tupo katika mchakato wa kuona kama inawezekana suala la #BASATA inakabidhi Tuzo kwa kampuni au taasisi nyingine ili iendeshe, hilo lipo kwenye uongozi wa juu wa BASATA, muda utakapofika litawekwa wazi.

Waliokuwa wakifanya kazi kwenye mchakato wa Kamati ya Tuzo walikuwa katika mazingira ambayo si ya rushwa wala hakukuwa na ushawishi wowote wa aina hiyo.

Maoni ya Sky Walker (Fredrick Bundala, Mdau wa Muziki)
sky walker.jpg

Picha: Sky Walker (Fredrick Bundala, Mdau wa Muziki)

Sky Walker (Fredrick Bundala, Mdau wa Muziki): Mfumo wa Wsanii kutuma maombi siuungi mkono kwa kuwa kiwanda chetu bado ni kidogo tofauti na hao wengine wa nje ambao wanatumia mfumo huo ambao unatumiwa na BASATA

Malalamiko huwa yanaanza pale tu wanaowania tuzo wanapojatwa, nilishiriki katika ile Kamati ya kwanza, niliona jinsi ambavyo mambo yalivyokuwa nayaenda ndivyo sivyo.

Mfano Tuzo ya Waandaaji wa Video Bora za Mwaka walioteuliwa hawakuwa na uhalisia wa kile kinachoendelea kwenye Kiwanda cha Muziki.

Kitendo cha wasanii wengi kutuma wawakilishi inamaanisha kuna tatizo, hali hiyo haikuwepo zamani, nashauri tuendelee na mfumo kama wa zamani wa kuachia Kamati ifanye kazi yake na kuanza Wasanii kujipendekeza.

Tuzo za sasa zimekuwa kama warsha, hakuna stori, hakuna shamrashamra nyingi mfano nani kavaa nini na vitu kama hivyo, hii ni burudani lazima mambo yanatakiwa kuchangamka.

Nashauri BASATA wanaweza kutangaza tenda, makampuni yakitokeze kuleta mawazo na kuibadili, ile hali ya 'showbiz' haipo tena, lakini #BASATA hawatakiwi kukata tamaa, tunawapenda na tunazihitaji tuzo.

Maoni ya Bazo Komu
1683818998008.png

Picha: Bazo Komu (Mdau wa Muziki)

Bazo Komu (Mdau wa Muziki): Tuzo za Mwaka huu nilizona siku moja kabla ya kufanyika, hakukuwa na matangazo wala utambulisho mkubwa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Ni lazima BASATA wajue kuwa Watanzania wanaupenda muziki lakini haujui kwa vipengele ili unaposema unampigia kura Msanii Bora wa Mwaka ajue sisa sahihi za mtu anayetakiwa kupigiwa kura.

Pamoja na yote, Wasanii wa Tanzania wanalalamika sana, wanashindwa kutambua kuwa tumewabeba sana japo wanastahili kubebwa.

Kitendo cha Wasanii kususa si sawa, tunapenda kujifananisha na Uingereza au Marekani, wenzetu wapo mbali sana. BASATA ni jukumu lao kuwabeba lakini nao Wasanii wabebe, wapunguze malalamiko.

BASATA wanatakiwa kuelewa Wataalamu wa Muziki ni kina nani na ambao wanaweza kupangilia Muziki Mfano vipengele vya Mwaka huu vilikuwa na changamoto hakukuwa na utaratibu mzuri wa kupangilia, pia inashangaza wakati huu ambapo kuna maendeleo mengi ya Teknolojia malalamiko ni mengi kuliko ilivyokuwa zamani.

Bila kumpa Msanii chochote kwake yeye anaona haina maana, hata darasani Mwanafuzi anaposhinda anapewa kitu fulani cha kuonesha kazi yake imethaminiwa

Mfano Wasanii walioshinda na wale waliobaki nyumbani hakuna tofauti, hivyo nashauri BASATA ikiwezekana watafute wadau nje ya wao wanaoweza kuwekeza kwenye Tuzo.

Natoa ushauri kwa BASATA, wasiweke waongozaji wote katika kapu moja, kuna waongozaji wa aina tofauti, waangalie hicho kipengele kwa kuwa wataishia kuwapa waongozaji walofanya video nyingi bila kujali ubora.

Maoni ya Vitali Maembe
maembe-data.jpg

Vitali Maembe (Msanii): Uwepo wa Tuzo ni jambo zuri sana kwenye Sanaa, kwa kuwa Tuzo hizi ni za Taifa basi nashauri Serikali kuwekeza nguvu zaidi kwa kuwekeza

Si Tuzo za watu maarufu bali watu muhimu wanaoimba katika ngazi mbalimbali na kuelimisha na kuburudisha jamii.

Unapomnyanyua mtu fulani katika jamii jua kuwa unawanyanyua watu wengine wanoona kile kinachofanyika

Ijulikane Tuzo si pesa lakini inatakiwa ithaminishwe, Serikali inatakiwa kuwekeza zaidi kwenye mchakato wa kuelekea Tuzo zenyewe.

Unapomwambia mtu achague msani funani una uhakika gani kama amemuona au amemsika? Inatakiwa kuwe na namna ya kuweza kutengeneza mazingira ya kuwafanya Wasanii waonekane na wasikike

Maoni ya Foby (Msanii)
1683824346146.png

Picha: Foby (Msanii)

Foby (Msanii): Nilipeleka wimbo wangu lakini sikupata bahati ya kuteuliwa kuwemo kwenye Tuzo, naamini muda utafika zamu yangu itafika

Napongeza Serikali kwa hatua ya Tuzo, niliwahi kushauri kwa BASATA kuwa hawatakiwi kuishia kufungia na kuonya wasanii, wanaweza pia wakawa wanawapongeza pindi Wasanii wanapofanya vizuri, nadhani hilo wanalifanyia kazi.

Hakuna Tuzo ambazo hazina lawama Duniani lakini kwa uelewa wangu mdogo Serikali wafanya utafiti wa kutuma watu wakajifunze katika Tuzo ambazo hazina lawama nyingi ili wajifunze wenzetu wanafanyaje

Wasanii nao hawana shukrani kwa mashabiki, kuna wengine wanashinda lakini hawapati nafasi ya kuwashukuru pindi wanaposhinda, ilitokea Mwaka jana na hata Mwaka huu pia

Maoni ya Wadau wengine wa Muziki
PATRON: Tunatakiwa kuangalia wenzetu waliotuzidi ili tujifunze kuhusu Tuzo, sio lazima tupite ugumu uleule ambao walipitia wao.

Kwizela Aristide: Inavyozungumzwa ni kama vile huko nyuma hakukuwa na malalamiko, Hapana yalikuwepo labda kuna utofauti tu wa aina ya malalamiko.

Tuzo zote huwa zina malalamiko hata hizo za nje pia, ni kama ilivyo kwenye mpira wa mguu kwa kuwa kila msanii anakuwa na watu wake nyuma wakiwemo mashabiki.

Kwizela Aristide: Inavyozungumzwa ni kama vile huko nyuma hakukuwa na malalamiko, Hapana yalikuwepo labda kuna utofauti tu wa aina ya malalamiko

Tuzo zote huwa zina malalamiko hata hizo za nje pia, ni kama ilivyo kwenye mpira wa mguu kwa kuwa kila msanii anakuwa na watu wake nyuma wakiwemo mashabiki.

Kwizela Aristide: Nimewahi kushiriki kwenye Akademi, huko nyuma ilifikia hatua inahusisha wanachama 200, ndani yake walikuwa watu wanaoujua muziki vizuri, hivyo ukitaja kipengele fulani walikuwa wanakijua kwa undani

Ilipofika siku ya kutaja washiriki wanaowania bado kelele zilikuwa zikiibuka, majina yakishatajwa ni lazima malalamiko yatokee kiasi ikafikia baadhi ya wasanii walikuwa wakijitoa, hivyo kinachoendelea sasa kuhusu malalamiko si kitu kipya.

Kwizela Aristide: Kuna kauli kuwa kulikuwa na rushwa, ni vigumu kuwa na uhakika na hilo kama huna ushahidi, kipindi kile Wasanii walipewa ‘code number’ na matokeo yalikuwa yanaoneshwa kwa Kamati kabla ya kutangazwa.

John Kitime (Mwanamuziki Mkongwe): Katika tuzo zilizopita hivi karibuni, Majaji walikaa siku tano, baada ya hapo tukaanz akuzungumza kuhutu Tuzo zijazo.

Maoni mengi yanayotolewa sasa yalizungumzwa katika vikao baada ya Kamati kumaliza kushughulikia Tuzo zilizopita.

Bob Eugen (Mdau wa Muziki): Inatia aibu kusikia kwenye Kamati ya Tuzo kuna wataalam wa muziki lakini majina ya wanaowania Tuzo yanapotoka unaona vitu ambavyo hautegemei

Mfano, hakuna kitu kirahisi kama kupata Wimbo Bora wa Mwaka, si wanaangalia ‘trending’, mbona hilo lipo wazi.

Rage Yasini (Mdau): Kurasa na mitandao yote ya BASATA lianzishe utaratibu wa kuwatangaza Wasanii wetu hasa wakati wa kuelekea katika Tuzo, hiyo inaweza ikawatangazia hata shoo au kazi zao pindi wanapokuwa nje ya Nchi, lengo ni kufanya Wasanii wajulikane zaidi

Tunapotangaza Tuzo za Tanzania maana yake ni kuwa tunatakiwa kuwa na mtu au watu wanaofanya vizuri Tanzania.

MDAU JFSpaces: Mfumo wa kupendekeza washiriki 'online' nao ni changamoto. Mara ya mwisho 'servers' zilikuwa 'greyed out'. Wakati mwingine unakuta sehemu ya category automatically limewekwa jina lako na hauna uwezo wa kubadilisha option iko fixed. Sehemu ya kuchagua aina ya tuzo unayowania unakuta ndio umepewa category ya muziki unaoimba.

Tatizo hili linaweza likafanya ionekane watu hawataki kuwania tuzo, kumbe wamejaribu ila mfumo umekuwa mbovu. Mpaka kuna muda tukawa tunafikiri kuwa kuna watu wao special ambao wamewachagua hivyo wengine wamewekewa ukuta ili washindwe. Suala hili hadi BASATA tuliwafikishia lakini hatukupewa majibu.

MDAU JFSpaces: Tuzo zitenganishwe na Kampeni za Siasa, tukio zima kugeuka kuwa tafrija ya Kupongeza Serikali na blah! blah! zisizo na tija ni moja ya vitu vinavyopoteza mvuto wa Tuzo hizo Wasimamizi wa Kamati wapunguze/waache u 'chawa', Kamati zisimamiwe na Watu wenye uelewa wa Muziki katika vipengele husika, Mfano: Bill Nas kuwa Mwanamuziki Bora wa Hiphop wa Kiume ilikua ni kituko cha Mwaka.

HITIMISHO
Maoni ya Mrisho Mrisho (Mratibu wa Tuzo za Muziki Tanzania kutoka BASATA):
Asante sana kwa mawazo yenu yote tunayachukua na kuyafanyaia kazi. Jamiiforums imetufungua kwamba tunaweza kufanya vvikao vingi na tathmini kubwa zaidi
 
Tuzo zisimamiwe na watu wanaojua mziki.

Tuzo nyingi naona zinaenda kwa watu wasio na sifa au mziki usio na sifa

Mfano kipengele cha muziki bora unakuta tuzo imeenda kwa mziki ambao ulivuma sana.

Watayarishaji wa tuzo hawajui kutofautisha kilichovuma na kilichokuwa bora, wao wanaona kilichovuma (kwenda viral sana) ndio kilicho bora.

Nimeona nyimbo nyingi ambazo zimepata umaarufu mkubwa na kuteka social media kwasababu ya matusi ya kimafumbo ambayo vijana wengi wakileo ndio wanapenda kuyasikia kwenye nyimbo.

Sasa nyimbo kama hiyo kutokana na kuwa maarufu unakuta unakuja kunyanyua tuzo ya nyimbo bora, ilihali maudhui yake ukiyakagua hayana ubora.
 
Tatizo ni kundi fulani la watu wanahisi wao ni bora hivyo wanataka wao ndo wapewe kipaumbele.

Serikali iachane na mambo ya Tuzo
 
Jambo jingine ambalo linatakiwa kuwekwa wazi ni thamani ya tuzo.

Ifahamike rasmi kuwa tuzo ina thamani ya shilingi ngapi, ili watu wasiishie tu kupewa kile kimbao na kukiweka kabatini bila kupata pesa yeyote.

Otherwise wawe na tuzo ambayo inakuwa na madini, mtu awe ana option ya kuweza kui convert kuwa pesa au akitaka kuiacha kama kumbukumbu iwe ni uamuzi wake.

Bila hivyo itakuwa ni kazi bure na ndio maana wengi hawaji nominee kwasababu tuzo hazina thamani yeyote nje ya sifa tu.
 
  1. Tuzo zitenganishwe na Kampeni za Siasa, tukio zima kugeuka kuwa tafrija ya Kupongeza serikali na blah blah zisizo na tija ni moja ya vitu vinavyopoteza mvuto wa tuzo hizo kwani.
  2. Wasimamizi wa kamati wapunguze/waache u chawa, kamati zisimamiwe na watu wenye uelewa wa muziki katika vipengele husika, Mfano Bill nas kuwa mwanamuziki bora wa Hiphop wa kiume ilikua ni kituko cha mwaka.
 
Na Safari hii wameamua kuwatega wachafu kw kuwapa tuzo za kutosha na jmaa wameshangilia sn bila kujua ni mtego wa kuwavuta Kwenye njia maana wao ilikuwa ni kukandia tu wakat wote
 
Kitu kingine ni maswala ya siasa yamekuja kuvuruga hizi tuzo na kuonekana ni kitu fulani cha kitabaka.

Msanii kwasababu ana foundation yake ambayo kuna mwana siasa ambaye anam-fund unakuta msanii huyo amechukua tuzo ambayo hata hakustahili.

Kuna wasanii mara ya mwisho kutoa nyimbo ni zaidi ya miaka 2 iliyopita, na katika hiyo nyimbo ya mwisho bado haikuwa nzuri, lakini unamuona kabeba tuzo ya msanii bora wa mwaka, msanii bora wa kiume, na nyimbo bora ya mwaka.

Hiyo yote ni kwasababu ya kutengeneza ushkaji na wanasiasa ambao wana influence kwenye boards za tuzo.
 
Watuangalie na sisi wasanii underground kwenye kile kipindi chetu pendwa cha ITV
kula chuma hiko
 
Uzuri nshashiriki academy za tuzo hizi zaidi ya mara 3,Tatizo kuna wasimamizi vilaza wengi sana,sijui mnawatoa wapi,malalamiko yanazidi kila siku,heri uwekwe utaratibu wa taasisi binafsi kuomba tenda,Tuzo wapewe Wanaojua kuandaa shughuli.Mbona zilivyokuwa chini ya kampuni ya Kilimanjaro ilikuwa afadhali kuliko Sasa?Tatizo vitu vya serikali yangu ni Bora liende.
 
Mfumo wa kunominee online nao ni changamoto

Mara ya mwisho servers zilikuwa "greyed out"

Sometimes unakuta sehemu ya category automatically limewekwa jina lako na hauna uwezo wa kubadilisha option iko fixed.

Sehemu ya kuchagua aina ya tuzo unayowania unakuta ndio umepewa category ya mziki unaoimba.

Tatizo hili linaweza likafanya ionekane watu hawataki kuwania tuzo, kumbe wamejaribu ila mfumo umekuwa mbovu.

Mpaka kuna muda tukawa tunafikiri kuwa kuna watu wao special ambao wamewachagua hivyo wengine wamewekewa ukuta ili washindwe.

Swala hili hadi BASATA tuliwafikishia lakini hatukupewa majibu.
 
Kuna namna siasa imeingia kwenye muziki, tuzo za sanaa lakini shughuli nzima ni serikali serikali serikali.

Kuna muda siasa zikae kando sio kila jambo ni lazima siasa ihusike kwa 60%.

Kingine ni siku yenyewe, ratiba iliharibiwa sana na watu dizani ya joti, steve nyerere na watu kama hao mpaka wengine tukaacha hata kufatilia.

Waambiwe mapema hao wanaotangaza washindi jukumu lao ni lipi, mtu anaongea dakaki 4 kabla hajamtangaza mahindi na bado akimtangaza anapokonya kipaza kwa mshindi ili amalize kuongea tena yeye.
 
Mjadala utafanyia leo kuanzia saa 11 jioni
Nasubiri kwa hamu nimeweka alarm kabisa ili ukianza tu nianze nao, nataka kujua wanatumia vigezo gani kuwapata washindi wa hizo tuzo maana naona kama kuna watu wanapewa na hawastahili na kuna wanaostahili hawapewi
 
Wasanii mbali na kutoa burudani, wana mchango wao katika kuwaunganisha Wananchi pamoja. Pamoja na yote haya, muziki ni ajira yao, ndicho kinachowaingizia kipato na kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali

Sasa siasa na mapichapicha yanapotokea kwenye Tuzo, inawavunja moyo kwa kiasi fulani. Michakato ya upatikanaji washindi katika Tuzo za Muziki ihusishe wanaoufahamu vizuri. Tusiweke siasa kwenye masuala ya sanaa!
 
Back
Top Bottom