Wana bodi salamu
Nasikitika taifa letu linapoelekea, inaonesha tunaacha mambo ya msingi na matatizo ya msingi kama taifa na kurukia rukia mambo na kutafuta umaarufu binafsi kwa baadhi ya viongozi
Suala la elimu bado ni tatizo kubwa katika nchi yetu hasa katika shule za umma. Tunaona mikoa yenye huduma karibu zote kama vile Dar es salaam, ndiyo iliyoongoza kwa kufanya vibaya zaidi. Serikali itafakari imekosea wapi katika suala la elimu na kutafuta ufumbuzi. Ikae na wataalamu wa elimu waliopo eneo la tukio (walimu) kuliko kukaa na kuhangaika na ripoti za akina Benson Bana na Kitila Mkumbo
Pia kuna suala la maji katika baadhi ya miji yetu
Uongo na kudanganya watu hakutatusaidia sisi kama taifa. Tushughulike na matatizo ya nchi kwa sasa, yapo, ndiyo yapo matatizo ya msingi kabisa ya kushughulikia.
Matatizo mengine ni usafirishaji kwa baadhi ya maeneo hasa vijijini. Hatukuwa na haja ya kuwekeza katika usafiri wa anga ambao ni usafiri wa wachache kwa hapa kwetu na si USAFIRI WA WANYONGE bali ni usafiri wa matajiri na 'wenye nazo'. Kuna barabara nyingi sina hali mbaya ingawa tunaaminishwa kwamba barabara zote zinasounganisha halmashauri za miji yote sipo kwa kiwango cha rami. Jambo hilo si kweli hata chembe.
Kwa nini isishughulike na uwekezaji mkubwa katika kilimo cha kisasa na hatimaye kupata malighafi za kutosha kisha kupanuka kiviwanda.
Kwa nini kama taifa tusiwe na sera ya pamoja, lengo la pamoja ambapo wananchi na viongozi wote tutashirikiana kulitekeleza.
Kwa nini leo kila kiongozi ana lake, mara madawa ya kulevya, mwingine kule mashoga, mwingine kauli za uchochezi. Kwani kipaumbele chetu hasa kama taifa ni nini!? Ni kushughilika na wachochezi tu!!!?
Nafikiri kama taifa, tungetafuta namna bora ya kuyakabili matatizo yetu ya kitaifa.