Tuwakumbuke marapa waliotisha kwenye bendi za Congo... Tutu Kaludgi na wengineo.

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
12,842
28,816
Kama shabiki mkubwa wa muziki nimeona leo niandike kitu tujikumbushe watu walionogesha sana muziki wa Congo... Marapa... hawa jamaa walikuwa wanafanya sebene zinoge. Ninaandika huku nikiusikitikia muziki wa dansi ukiwa hauna nguvu kabisa kiasi kwamba wanamuziki wa Bongo Fleva na wanigeria wanaonekana wakubwa sana. Pamoja na changamoto zote bado kuna wanamuziki wa bolingo ambao wameweza ku-maintain hadhi zao. Koffi, Fally, Ferre na kina Fabregas bado wako vizuri.

Wafuatao kwangu mimi ni marapa bora kabisa kuwahi kutokea;

1. ROBERTO EKOKOTA; Huyu mzee msikilize kwenye albamu za mwanzo mwanzo za Wenge BCBG kabla hawajatengana. Alifanya vyema. Aliigwa style ya uimbaji na marapa wa bendi zingine. Wanasema hakuendelea kuimba kutokana na matatizo ya kiafya.

2. TUTU KALUDGI; Huyu mzee nae ni kutoka familia ya Wenge BCBG. Tutu Kaludgi huwa ana uimbaji wa kipekee sana. Msikilize kwenye albamu Pentagone, Titanic, Internet na TH. Kama ilivyokuwa kwa Roberto hata Tutu aliigwa mno namna ya uimbaji wake hadi waliomwiga akawaita Kalunjists. Tutu Kaludgi ni mtumishi mwema na mwaminifu wa Wenge BCBG kwasababu hakuwahi kuhama bendi.

3. BILL CLINTON: Rapa wa Wenge Maison Mere ya Werrason. Huyu alitikisa mno mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwenye albamu ya Solola Bien. Nae pia alikuja kitofauti sana kiasi kwamba ilibidi Koffi Olomide atafute rapa aitwaye Kerosene ili kurap kama Bill Clinton kwasababu style yake ndo ilikuwa inatrend. Sifa nyingine ya Bill Clinton ni uwezo wake mkubwa wa ku-dance. Kusakata sebene ni mtu hatari. Kwenye Live Shows alikuwa akifanya kazi kubwa mno. Nenda You Tube ukafaidi.

4. CNN ALLIGATOR: Enzi za ujana wake CNN aliwasha moto hasa kwenye albamu ya Attentant na Force De Frappe ya Koffi Olomide & Quartier Latin. Ni ile Quartier Latin ya kina Fally Ipupa, Soleil Wanga, Fely Tyson, na wakali wengine. CNN hakuwa nyuma kwenye kuyarudi masebene. Kwenye show alikuwa haboi. Kwenye show ya tuzo za Kora 1999 alifanya kazi nzuri hadi Hayati Nelson Mandela alishindwa kujizuia na kuwashangilia.

5. KILA MBONGO: Ni rapa wa Extra Musica aliyetikisa mno kwenye albamu nyingi za Extra ila anakumbukwa zaidi kwa alivyorap kwenye Losambo, Etat Major na Amnistie Shalai. Ni miongoni mwa wacongo wachache ambao mkorogo uliwakubali. Kama ilivyo kwa Tutu Kaludgi huyu Kila Mbongo nae ni mtumishi mwaminifu kwasababu ya kutokuhama bendi.

6. CELEO SCRAM: Mimi naweza sema Celeo Scram alikuwa rapa mzuri sana ila uwepo wa Bill Clinton pale Wenge Maison Mere ukawa unamfanya awe chaguo la pili. Kwenye albamu zote za mwanzo za Werrason kashiriki vizuri. Baada ya Bill Clinton kuondoka Wenge huyu Celeo alipata nafasi ya kujiachia na kufanya vizuri kwenye albamu Alerte Generale. Naye alidumu sana pale kwa Werrason.

7. FALLY IPUPA: Kamsikilize kwenye wimbo Generation Bercy. Kafanya vyema sana mle.

8. GENTAMCYNE: Humu JF kuna member mmoja kichwa moto sana aliamua kujipa jina la huyu rapa kwa sababu anamkubali. Member huyu ndo mwasisi wa neno popoma. Gentamcyne ni rapa mkali sana kuwahi kutokea kwenye bendi ya Wenge BCBG chini ya JB Mpiana.. kashiriki kuanzia albamu ya Internet, TH na nyinginezo. Hadi leo ni mfanyakazi wa Wenge BCBG ila umri umeenda sana.

9. SABARTY BRIGADE: Sikiliza dude Efrakata ya Koffi Olomide ndo utaelewa balaa la Brigade. Alikuwa akishirikiana Bebe Kerozene. Alikuja kuhamia Wenge Maison Mere ambako pia alifanya vizuri.
 
Nkonzi wa Nkonzi wa The Big Stars ya General Defao R.I.P. Msikilize kwenye Album ya Bana Congo na Wimbo Phyli na Le Guerre de 100 Ans zote za Defao utakubali.
Bill Clinton kwenye “Force D’intervention Rapide “ utampenda
 
Solola bien by Wenge Maison Mere

Force d’Intervention Rapide ya Wenge Maison Mere ilikua hatari. Ilikua ni kujibu Titanic ya JB Mpiana au Titanic ilikua ni kujibu Force d’Intervention Rapide ya Werasson. Hapo Bill Clinton ( Werasson) na Tutu Kaludji( JB Mpiana) walifanya kweli
 
Sielewi sana rapa kwenye ngoma za dansi anakuwa anafanya vitu gani. Mfano kwa Koffi, Suzuki na yule alieimba na Koffi kwenye Alidor wana tofauti gani?
 
List yangu ya Maatalaku Bora wa muda wote kwa mziki wa Kongo..
1, Roberto Ekokota
2, Gentamicine
3, Bill Clinton
4, Kila mbongo
5, Arafati Wanya
 
1. Bill Clinton Kalonji
2. CNN Alligator
3. Celeo Scram
4. Totou Caludji
5. Mboshi Lipasa
 
1. Bill Clinton Kalonji
2. CNN Alligator
3. Celeo Scram
4. Totou Caludji
5. Mboshi Lipasa
A-4854971-1601659530-4227.jpg
A-4854971-1514214602-7485.jpg
A-4854971-1601659321-8049.jpg
 
Woote hao nawakubali, ila mie kila mbongo namkubali zaidi, kazi zake alizofanya ni hatari na nusu. Losambo, fredy Nelson, shalai na nyinginezo.

Ila ngoma niipendayo zaidi ni effrakatta waliorap mule walituliza vichwa.
 
Back
Top Bottom