Tutegemee athari zipi kiusalama nchini Tanzania baada ya Rais Ruto kutangaza Hali ya hatari?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
18,778
29,101
Salaam,Shalom!!

Ile Hali ya wanasiasa kujifanya viziwi Kwa kutosikiza MAONI ya wananchi ambao ndio hasa boss wao, imesababisha Bunge kutekwa kuchomwa na waandamanaji baada ya Polisi kuzidiwa nguvu na namba.

Swali: Tutegemee athari gani kiuchumi,Kijamii, na hasa KIUSALAMA mipakani Kwa siku zijazo baada ya Rais Ruto kutangaza Hali ya hatari hii leo?

Karibuni 🙏
 
Kwanza athari ya kwanza ambayo tunatakiwa tuwe macho zaidi ni wahalifu wakubwa hasa magaidi mda huu ndio wanaweza penyeza watu wao wakati watu wapo busy kuangalia maandamano, jambo jingine ni wageni wa kuingia kwetu kutokea Kenya na wakaleta tabia zisizo la mwisho kabisaa viongozi wetu wajifunze na kuchukua hatua madhubuti ya kuongea vizuri na wananchi na kutekeleza majukumu yao kwa weledi na sio vitisho
 
Salaam,Shalom!!

Ile Hali ya wanasiasa kujifanya viziwi Kwa kutosikiza MAONI ya wananchi ambao ndio hasa boss wao, imesababisha Bunge kutekwa kuchomwa na waandamanaji baada ya Polisi kuzidiwa nguvu na namba.

Tutegemee Hali Gani KATIKA USALAMA mipakani Kwa siku zijazo baada ya Rais Ruto kutangaza Hali ya hatari?

Karibuni 🙏
You are exaggerating things
 
Hii hali ya Hatari aliyoitangaza Rutto sidhani kama itazidi Wiki moja, lakini kama ndugu zetu Wakenya wakihofia Maisha yao kuwa hatarini kutokana na State Apparatus kuwawinda kama Digi Digi basi TUNAWAKARIBISHA TANZANIA waje kuomba HIFADHI.

KARIBUNI SANA NDUGU ZETU WAKENYA hata kama Kaugali ni nusu tutakula wote.

Sisi pia TULIWINDWA kama DIGI DIGI na DIKTETA MAGUFULI Ndugu zetu Wakenya wakatukaribisha tukashea nao Sukuma Wiki.
 
Salaam,Shalom!!

Ile Hali ya wanasiasa kujifanya viziwi Kwa kutosikiza MAONI ya wananchi ambao ndio hasa boss wao, imesababisha Bunge kutekwa kuchomwa na waandamanaji baada ya Polisi kuzidiwa nguvu na namba.

Tutegemee Hali Gani KATIKA USALAMA mipakani Kwa siku zijazo baada ya Rais Ruto kutangaza Hali ya hatari?

Karibuni 🙏
Kwa kweli na ki-UKWELI hali haitakuwa nzuri tena kama tulivyo zoea. Mabadiliko ni lazima yatakuwepo. Yanaweza kuwa mabaya au mazuri kutegemea mtizamo wa mtu. e.g. Subjective.
1. Kwa waliokuwa wanajiendea kuingia na kutoka kiholela Kenya bila ya pass sasa itakuwa sivyo tena. Utaratibu utabadilika.
2. Jeshi kusimamia Utendaji i.e. Hali ya Hatari manake hakuna MASIHARA tena. Ukienda kinyume unaweza kubutuliwa na hakuna pa kwenda kulalamika. Muda wa kuzurura/kutembea kwa Starehe utadhibitiwa sana au hakuna kabisa.
Huko kwa jirani(Kenya) sisi waTz tunayo maslahi binafsi mengi na muhimu e.g. Wapo Wanafunzi kutoka Tz wanaosoma Kenya, Wapo Wafanyabiashara wa kiTz hupeleka na hurudi na mizigo ya Bidhaa-(bidhaa, magari na madereva); huko Kenya waTz tuliweza kupata huduma za kiafya n.k, n.k
Kwa mantiki hiyo Watanzania (wabongo) waliokuwa wananufaika na kuwepo kwa jirani yetu; kwa vyovyote vile sasa wataathirika kutokana na Kutangazwa kwa HALI YA HATARI nchini Kenya.
Endapo hali itazidi kuwa mbaya tunategemea pia kupokea wakimbizi kutoka Kenya. Wakimbizi hao watahitaji huduma muhimu za kibinadamu - chakula, huduma za Afya na Malazi. Lakini pia wakimbizi watakuja na Tabia zao nzuri au mbaya yakiwemo na maradhi ya kuambukiza.
Kwa kuwa hali itakuwa ni Tete(Instability/unstable state), Maadui zetu wa ndani na nje ambao pia hatuwajui wanaweza kuitumia hali hiyo kufanya yao.
Wadau wataendeleza kwa kuchangia hoja.
 
Hii hali ya Hatari aliyoitangaza Rutto sidhani kama itazidi Wiki moja, lakini kama ndugu zetu Wakenya wakihofia Maisha yao kuwa hatarini kutokana na State Apparatus kuwawinda kama Digi Digi basi TUNAWAKARIBISHA TANZANIA waje kuomba HIFADHI.

KARIBUNI SANA NDUGU ZETU WAKENYA hata kama Kaugali nusu tutakula wote.

Sisi pia TULIWINDWA kama DIGI DIGI na DIKTETA MAGUFULI Ndugu zetu Wakenya wakatukaribisha tukashea nao Sukuma Wiki.
Na tulipofungiwa Jamiiforum yetu walitukaribisha Kenya talk huko tuliishi poa tu japo kuna waliotuita takataka.
 
Salaam,Shalom!!

Ile Hali ya wanasiasa kujifanya viziwi Kwa kutosikiza MAONI ya wananchi ambao ndio hasa boss wao, imesababisha Bunge kutekwa kuchomwa na waandamanaji baada ya Polisi kuzidiwa nguvu na namba.

Tutegemee Hali Gani KATIKA USALAMA mipakani Kwa siku zijazo baada ya Rais Ruto kutangaza Hali ya hatari?

Karibuni 🙏
Tutegemee yafuatayo:

1. Chura kiziwi, yule mjinga hatimaye masikio yake yanaweza kufunguka na kuelevuka. Nasema ni mjinga kwa sababu kwa nafasi yake kama kiongozi mkuu wa nchi hii, ni ujinga na ukosefu wa hekima na busara tu kulikomfanya atamke maneno hayo mbele yaumma na yatamrudi daima mpaka ashike adabu yake na kutubu!

2. Mbegu hii kuingia Tanzania na itakuwa balaa kuliko kinachoendelea Kenya. Ogopa sana mtu mpole, mkimya na mvumilivu anapochukizwa na jambo na kuamua kupambana. Watanganganyika ni wapole na wavumilivu sana. Wamevumilia ujinga na upumbavu mwingi kwa miaka mingi sana toka kwa CCM na serikali yao tangu uhuru 1961. Sasa enough is enough
======================================

HATUA ZA TAHADHARI ZA KUCHUKUA SASA

1. Ondoa viongozi wote wajinga wajinga na wasiojua wajibu wao mfano RC wa DSM, Arusha, Waziri wa Fedha na Rais mwenyewe (Samia Suluhu Hassan) hawafai

2. Ondoa viongozi wote wezi na wabadhirifu wa fedha za umma. Waziri wa Fedha, Kilimo, Nishati na Madini nk nk

3. Vunja Bunge hili. Hili sio Bunge la wananchi Bali ni Bunge la CCM na serikali. Hili Bunge ndilo litakuwa chanzo cha machafuko nchi hii. Kwanza wote hawakuchaguliwa, waliwekwa tu na mwenzao Hayati Rais John P. Magufuli ambaye yeye tayari ameshakufa. Hata hawa wote 99% wanastahili adhabu ya kifo kwa mwenendo na matendo yao!

Itaedelea..............................
 
Back
Top Bottom