Kiwalani finest
Member
- Jul 6, 2024
- 91
- 64
Mgonjwa Akiwa ICU Huhitaji maombi. Tusichoke kuwaombea wale wote wanaotamani kuwa wanasiasa.
Mwanasiasa wa ukweli ana bidii ya kusoma ili kujua misingi ya nchi, kisha kwa imani yake kumuomba Mwenyezi Mungu kuiishi misingi hiyo huku akiwa mnyenyekevu na mtiifu. Mwanasiasa huyu anaitekeleza kwa vitendo ibara ya 08(1) a, b, c, d ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, toleo la 2005. Anazingatia pia ibara ya 26(1) ambayo inasomwa kwa pamoja na ibara ya 09 a, b, kutokana na hofu ya kuivunja ibara ya 09 h inayoshereheshwa na ibara ya 13(1), kwa kuzingatia ilani ya CCM ya mwaka 2020 ukurasa wa 01, ibara ya 04, inayolazimishwa utii wake na ukurasa wa 08 ibara ya 10 na 11, kwa sababu za msingi zitokanazo na utashi wa kurasa za 161-168.
Mtu ajiitaye mwanasiasa, aliyevalia akadamshi, akiwa na mionekano nadhifu kabisa kama vile ni kada, huku kichwani mwake akiwa na akili ya "shake before use"—nikimaanisha hajui lolote kuhusu ilani, katiba, kanuni, miongozo na taratibu—akibaki haelewi mifumo ya nchi, na kuapa viapo kwa kushika maandiko matakatifu huku akiwa hajui hata maandiko hayo yameandikwaje. Mtu huyu mwenye hasira muda wote, akiwafokea wenye utii kwa mifumo na kuwabeba maboya sambukile sambamba, ni hatari sana kwa ustawi wa nchi. Hatupaswi kuona aibu kumkemea, kwani mtu huyu ndiye mnyama hatari kuliko wanyama wote walao nyama katika ulimwengu.
Mnafiki, mzandiki mwenye kujitamkisha neno Mwenyezi Mungu ili kuwazuga mafukara wamuamini, lazima akemewe hadharani bila kificho. Hana tofauti na mgonjwa mahututi mwenye mionekano kwa nje kama yuko sawa, kumbe akiwa kaoza maini kwa ndani. Mwanasiasa huyu ndiye chanzo cha mmomonyoko wa maadili, huku akinawirisha ngozi yake ya kondoo aliyoivaa ili aendelee kuonekana kama kondoo, kumbe ni mbweha.
Nikashtuka katika ulimwengu wa kiroho huko ndotoni, nikiwaona wanasiasa wagonjwa wanaostahili kuwa ICU, ila wakiwa wanaonekana kwa nje kama makada wanaostahili heshima na kutuvusha, kumbe wameoza kifikra wakisubiri kunuka.