Tuongee kuhusu Dhuluma

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
14,777
42,955
Habari za asubuhi!
Leo nimeona ni vyema niamke na mada inayoitwa DHULUMA.

Leo naomba niiongelee dhuluma kwa level ndogo, hii dhuluma kwa level ndogo ni ile haswa baina ya mtu na mtu, au kikundi kidogo kwa mtu mmoja au mtu mmoja kwa kikundi kidogo.

Dhuluma (injustice) ni hali ya kumeza haki ya mtu mwingine kwasababu ya nafasi uliyonayo au mamlaka yako au kwasababu ya mamlaka ya ndugu / rafiki yako.

Mfano wa dhuluma ndogondogo
1. Kijana amefanya usaili wa kujiunga na jeshi la nchi yake kapata alama 80 kati ya 100 anaachwa na kuchukuliwa aliyepata alama 60 kwakuwa kijana huyo aliyepata alama 60 ni mtoto au Kiongozi au kampa fedha kiongozi.

Matokeo yake ni nini?
Matokeo yake ni mmoja atapata ajira na mmoja atakwenda kufanya shughuli yoyote ilimradi asife njaa. Kama maisha huyu mmoja yatamgaragaza na akakaa akakumbuka kuwa jina lake lilikatwa kwenye usaili na kuwekwa mwingine au hata asipojua kuwa alichezewa rough kwenye usaili lakini tu akawaza kuwa nilikosa kazi ya jeshi ambayo ingenifanya nimsaidie mama yangu na kuendesha maisha.

Ule uchungu moyoni mwake unamwamsha Mungu kwa hasira, Mungu huona na kujua siri zote. Ndipo Mungu kwakuwa anaitwa Mungu wa visasi anampeleka mission kijana wa upande wa pili huku mwenyewe akifurahia mamilioni ya UN, maana anajua akirudi tu atanunua gari ya kwenda kufanyia show up. Kumbe Mungu ameandaa watu wa kumwotea uhai wake (kumuua).

Kijana atakufa vitani familia itaumia, Mungu atatulia maana tayari ameshalipa kisasi, zoezi litakalofuata ni kuhamisha baraka za upande wa pili kwenda upande wa aliyedhulumiwa.

2. Watu wawili wanagombea shamba. Mmoja kwasababu ya uwezo wake wa kuongea na kujenga hoja au pengine ana uwezo wa kumuhonga hakimu mwisho atapatiwa shamba ambalo si haki yake.

Mungu wa haki siku moja atapitia file la ile kesi na kulipa kisasi. Ndipo matatizo watu huwajia bila kujua yametoka wapi . Wakati mwingine watu husema karogwa kumbe ni mkono wa Mungu.

3.Daktari au mfamasia wa umma anayechota dawa kwenye hospitali za umma na kwenda kuziuza kwenye duka lake huyo amedhulumu haki za maskini wazee na watoto ambao kimsingi wanapaswa kutibiwa bure.

Baadaye huambiwa dawa hii na ile zimeisha nenda kajinunulie, maskini atajichanga atanunua au atashindwa kuzipata kwakuwa ni ghari mwishowe atakufa.

Hasira za Mungu zitawaka siku moja atakapopitia lile file na ndipo mtu huanguka ghafla na kufa au kupata ajali na kuondoa miguu yake au kupooza milele.
4. Fisadi
n.k, n.k
Adhabu ya kumlipa dhalimu Mungu ndiye hupendekeza kwa uamuzi wake mwenyewe.

Anaweza kukichapa kizazi chako cha pili au cha tatu au wewe mwenyewe, na siku ya kisasa yeye Mungu ndiye huichsgua.

Cha msingi wewe dhalimu jua tu Mungu amekuweka kwenye kilengeo chake, huwezi kukikimbia kisasi chake. It's matter of time.

Ikimbie dhuluma, hasa dhuluma kwa asiye na nguvu/maskini.
Naongea katika Roho.
Mwenye sikio na asikie.
 
Back
Top Bottom