Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,323
- 152,136
Kwa mwenendo wa Bunge hili chini ya Spika huyu wa sasa,ni imani yangu tungekuwa na wanasiasa/mwanasiasa machachari na mwenye ujasiri kama Julius Malema kwenye Bunge letu,basi mpaka muda huu mchakato wa kutaka kumuondoa Spika madarakani ungekwisha aanza bila kujali utafanikiwa au laa.
Sijui tunasubiri kitokee nini ndio tuone umuhimu wa kubadili uongozi wa hili Bunge letu walau kwa kuonyesha tu hatuna imani na kiongozi wa taasisi hii.
Tumekuwa watu wa kulalamika tu kuanzia sisi wananchi wa kawaida,badhi ya viongozi wa wastaafu,n.k lakini hakuna hatua tunayochukua japo ni haki yetu kikatiba kufanya hivyo!
Unajua hata mtaani kama kuna sehemu ukipita huwa kuna mbwa ambao huwa wanabweka tu na hawang'ati na ukagundua udhaifu huo,basi kamwe huwezi ogopa kupita mtaa huo hata kama ni usiku wa manane.
Wameshagundua udhaifu wetu huu na ndio maana hawana hofu na pia ndio maana vituko au mambo ya aina hii hayaishi kwani wanaamin kelele zetu ni upepo tu ambao utapita kabla hawajaja na lingine.