JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,668
- 6,432
Akihojiwa na Katika Kipindi cha Dakika 45 cha ITV, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema “Sikuwahi kufuatwa na Mtu akaniambia anipe hela ili nisiwe na msimamo Fulani, safari hii nimefuatwa ndio maana imebidi nikemee hadharani.”
Bila kufafanua Watu au Mtu anayemzungumzia, Lissu amesema waliofanya hivyo walimfuata nyumbani kwake. Amesema “Kuna tatizo na linatakiwa kusemwa hadharani, hawakutaka niondoke CHADEMA walitaka nipunguze ukali, wanisaidie kuangaiangaika mfano sina gari…”
Soma Pia: Lissu: Abdul aliniletea rushwa nyumbani kwangu nikamwambia "Shenzi, kahonge wanaohongeka"