johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 96,005
- 168,413
Simba wa Kizimkazi mh Tundu Antipas Lisu amepeleka kilio chake kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia juu ya kutekwa na kupotea kwa kijana Deus Soka
Makamu Mwenyekiti huyo wa CHADEMA ametoa kilio chake ukurasani X
Ahsanteni Sana 🐼
======
Rais Samia, kijana huyu anaitwa Deus Soka; ni kiongozi wetu wa chama katika wilaya ya Temeke. Tarehe 26 Julai alikuja kunipokea Dar International Airport niliporudi safari ya Ulaya. Sasa, baada ya vitisho vingi, watu wako wamemteka nyara. Hajulikani alipo kwa zaidi ya wiki mbili
Waliomteka nyara wanajulikana. Ni watu wa kikosi kazi chenye makao makuu yake nyuma ya Kituo cha Polisi Chang'ombe, Dar es Salaam. Kikosi kazi hiki ni kundi la maharamia, hata kama wanajiita askari polisi au usalama wa taifa na wanalipwa mishahara kwa kodi zetu. Ni kundi haramu.
Kwa Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa kama ilivyo leo, wewe, Rais Samia, unahusika moja kwa moja & maharamia hawa. Sheria hiyo inasema wanawajibika kwako. Wote wako chini ya mamlaka yako kikatiba & kiutendaji. Mimi nasema wewe ndiye unayewatuma wafanye uharamia wao kwa wananchi.
Nakusihi kwa moyo wangu wote: usijesahau ya mtangulizi wako & kikosi kazi chake cha 'watu wasiojulikana.' Yeye alikufa huku damu ya Ben Saanane & ya Azory Gwanda & ya Simon Kanguye ikimlilia. Angalia yasije yakakufika yaliyomfika. Mrudishe Deus Soka & wenzake wakiwa hai & salama
Pia soma: Kuelekea 2025 - Watu Wasiojulikana: Malisa aelezea tukio la kutekwa kwa Deus Soka na vijana wengine wawili wa CHADEMA