LIVE TOKA MAHAKAMA KISUTU
Anaandika YERICKO
Tupo mahakamani, tayari Mh Lissu ameshaletwa Mahakamani,
Lissu anatetewa na wanasheria 17 wakiongozwa na John Mallya Peter Kibatala na timu nyingine toka makao makao makuu ya Chama.
Viongozi wote wa makao makuu wameshawasili,
Tunasubiri Hakimu tu aingie kwenye ukumbi wa mahakama...
UPDATES,
Tayari Hakimu Mh Jongoro anayesikiliza shauri ameshawasili, sasa ni utambulisho wa mawakili wa pande zote,
Kesi inaanza kusomwa,
Mwendesha mashitaka: Tundu Lisu anashitakiwa kwa makosa ya uchochezi, mnamo tarehe 28/06/2016 akiwa eneo la mahakama kwania ya kudhalau umma dhidi ya mamlaka yao walioyoichagua kihalali, alisema huyu dikteta uchwara lazima tumpinge kila kona"
Hakimu: Mshitakiwa, unakubali au unakataa?
Lissu: nakataa yote
Mwendesha mashitaka: Mh Hakimu ushahidi wa shauri hili umekamilika, tunaomba tarehe ya kuanza usikilizwa,
Hakimu: Mawakili wa utete mnalololote la kusema?
Wakili: Mheshimiwa kwamjibu wa kifungu cha sheria na.... Mshitakiwa kosa aliloshitakiwa linadhaminika, hapa tunao wadhamini na zaidi mshitakiwa ni mbunge na mwanasheria wa chama, hivyo anadhaminika, na zaidi mshitakiwa aliliripoti mwenyewe mbele ya polisi baada ya kuitwa tu kwa simu. Ni hayo tu mh
Mwendesha mashitaka: Mshitakiwa aliyembele yako, mnamo tarehe 28 mwenzi huuhuu alifikishwa mahakamani kwa kosa...... Aaah nimesahau sina nakala ya mashitaka, na wenzake watatu na kudhaminiwa. Hivyo akatenda kosa hili, huyu ana nidhamu mbovu, ameona kutenda kosa ni kawaida,
Hakimu: Kwanini unamhukumu kwa kosa ambalo mahakama hii haikumtia hatiani...na siajabu akitoka hapa atatenda kosa tena....
Wakili: Mh hakimu nashindwa kujua huyu wakili wa serikali anajipa kazi ya hukumu kwa kesi iliyopo mahakamani, nimshauri arudi kwenye kesi iliyopo mezani kwakuwa kesi ya nyuma ni tuhuma tu na sio hukumu inayoweza kutumika kama kielekezo hapa.
Mwanasheria: Mh huyu mtuhumiwa ni mzoefu wa kutenda makosa...... Watu wanaangua kicheko kwa kwa kwa...
Hakimu..... Wakili
Wakili: Kwanza Mh hakimu naomba ifahamike kwamba upande wa serikali wamekubali kuwa suala la dhamani liko wazi, hili liweke katika kumbukumbu... Haya anayoyaleta sasa huyu mwanasheria hayana msingi, kwani kwa mjibu wa vifungu vya sheria na.....na... Vinampa haki yakupata dhamana, izingatiwe kuwa katika dhamana ya kesi ya mwanzo hakukuwa na mashariti ya mtuhumiwa kutotoa maoni ama kutenda kosa nje ya lile.. Izingatiwe kuwa sababu za kukidhi dhamana tumeshazitoa
Hakimu: Mahakama inaamua kuwa mtuhumiwa apewe dhamana, wadhamini wa mtyhumiwa waje mbele...kuhakiki nyaraka zao
Mwanasheria: Anainuka... Mh Hakimu...
Hakimu: Mwanasheria tambua sehemu iliyosalia ni maamuzi ya mahakama, hivyo wadhamini njooni mbele.....
Kesi itatajwa tarehe 2/8/2016