Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 216
- 993
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema kuna mchezo haramu unafanyika kwenye utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nchini, na kama wahusika watabisha (watakanusha) tuhuma hizi basi atawataja hadharani.
"Kuna biashara inafanyika na mimi nitataja majina mtashangaa, kuna siku nitataja majina mtashangaa. Kuna watu wanapewa vibali anaambiwa hivi kwa kila kilo moja ya kibali cha kuagiza sukari nje lipa Tsh. 200. Tukikupa tani 30,000, ni kilo milioni 30, zidisha mara 200 ni Tsh. Bilioni 6."
"Mfanyabiashara analipa Bilioni 6 anapewa kibali cha kuagiza sukari, anaagiza sukari anakuja kuongeza yeye Tsh. 1000 juu, wewe unanunua sukari bei imeongezeka kwa Tsh. 1000 ya mfanyabiashara na 200 ya hii biashara ya huyu malkia na watu wake wa Ikulu."
Ameongeza "Kama kuna mtu anabisha anataka tutaje orodha ya viongozi wa kidini waliopewa vibali vya sukari, viongozi wa kidini, Shehe gani kwenye nchi hii ana duka la sukari, au askofu gani kwenye nchi hii ana duka la sukari? Anapewaje kibali cha kuagiza tani 35,000 za sukari afu yeye anaenda kuuza kwa wafanyabiashara anawaambia nipe mia mbili mia mbili kwa kilo, wakibisha na wabishe waone. "