- Source #1
- View Source #1
Nimesikia Tundu Lissu amekimbizwa Ulaya kulikoni jamani. Anaumwa nini tuambieni kilichomfanya kuacha mikutano na haraka haraka akakimbizwa nje ya nchi.
- Tunachokijua
- Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA ameendelea kuongelewa katika muktadha wa siasa nchini kwa mambo mbalimbali.
Leo Juni 24, 2024 kuna hoja inazunguka mtandaoni ikidai Tundu Lissu ni mgonjwa na kwa sasa ameenda Ulaya kutibiwa huku chanzo ugonjwa wake kikiwa hakijulikani
Ukweli ni Upi?
JamiiChek imefuatilia taarifa hii na kubaini kuwa haina ukweli.
JamiiCheck imewasiliana na Tundu Lissu ambaye amekanusha madai haya.
Akiielezea JamiiCheck kwa ufupi Tundu Lissu anasema:
Sijakimbizwa Ulaya Wala sijaacha mikutano ya hadhara. Nimemaliza ratiba yangu ya mikutano ya hadhara Singida Juni 20, 2024. Arusha nilienda kwa ajili ya mikutano ya Karatu na Ngorongoro tu. Nimerudi Dar jana usiku leo jioni nasafiri kwenda Ubelgiji kwa regular medical check up na mapumziko. Nitarudi baada ya mwezi mmoja