Pre GE2025 Tundu Lissu: Ili tuweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa kura!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,870
5,045
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumzia harakati za 'No Reform No Election' amedai kuwa "Ilituweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa kura"

"Watu wetu wa leo ni welevu kuliko miaka 10 iliyopita, mwaka jana muliweka wagombea wa nafasi zote zinazogombaniwa hapa Kibamba na sehemu kubwa walienguliwa, mkatumia nguvu kubwa kuwarudisha, wakarudishwa baadhi alafu siku ya tarehe 27 mkashughulikiwa vizuri zaidi, matokeo yakatangazwa kwa mitutu ya bunduki ndio maana hamna Mwenyekiti wa mtaa hata mmoja, sio kwasababu mmekuwa wajinga kuliko mlivyokuwa miaka 10 iliyopita ni kwasababu sasa hivi ilitushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao"

Lissu ameendelea kwa kusema: "Katika mazingira ya uchaguzi wa sasa ili tushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao, ili wasiweze kutumia bunduki zao kuingia vituoni kwa nguvu na kuchukua masanduku ya kura kwa nguvu,"

Lissu amehoji: "kama na sisi tukiwa na bunduki hiyo nchi itakuwaje?, patakua na pakukaa hapo?, ndivyo wanavyotaka?

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

 
Back
Top Bottom