Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,447
- 3,760
Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara, Tundu Lissu kuhusu kuitwa Mwanaharakati na sio Mwanasiasa kwahiyo hafai kuwa Mwenyekiti wa Chama.
"Mwanaharakati inatumika kama neno huna sifa, Wanaharakati maarufu wa dunia hii ni kama Julius Nyerere, Nelson Mandela. Yeyote yule unayemfikiria katika Afrika hii ambaye aliongoza mapambano ya mabafiliko alikuwa Mwanaharakati, alikuwa mchochezi, alikuwa mhaini…"
"Yeyote anayeniita Mwanaharakati zaidi ananipa heshima [ananiweka katika jengo moja na hao niliowataja na wengine wengi].. ni jina la heshima sio jina la fedhea"
"Ukiambiwa wewe ni Mwanaharakati sio Mwanasiasa… Mwanasiasa anaonekaka huyo ni muongo muongo, uwe mlaghai laghai, ukipewa unachukua unaweka huku alafu huku unajifanya msafi, maana yake ni mtu ambaye mswahili swahili asiyeaminika. Kwa maana hiyo napendelea waendelee kuniita Mwanaharakati wasiniite Mwanasiasa wa nipe nikupe, kuna mtu alikaa kwenye kiti hicho hicho akasema bwana nikupe uache kunisema sema, ningekuwa Mwanasiasa wa aina hiyo ningechukua mfukoni maisha yakaendelea"
Pia, Soma: