Tundu Lissu: Askofu Gwajima ndiye alikua mshenga wa Lowassa kuja CHADEMA

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,448
3,760
Wakuu

Tundu Lissu amesema Askofu Gwajima ndiye alikua mshenga wa hayati Edward Lowassa kwenda CHADEMA

Soma: Mdahalo wa Wagombea Uenyekiti CHADEMA Taifa

"Dkt. Slaa ndiye aliyemleta Edward Lowassa CHADEMA, ndiye aliyeanzisha hilo wazo, ndiye aliyeongoza timu zote majadiliano za CHADEMA kujadiliana na timu ya Lowassa na ndiye aliyeitisha kikao cha Kamati Kuu cha kumkaribisha Lowassa na ndiye aliyenipigia mimi simu nikiwa jimboni kwangu Singida, Mashariki tarehe 26, 27 kama sikosei ya Julai 2015 na kuniambia njoo tuna Kamati Kuu ya dharula kesho

"Na usiku wakati nasafiri kuja Dar es Salaam akanipigia simu kunambia kwamba Chama kimeuzwa alafu nilipokutana nae kesho yake na Mwenyekiti na Askofu Gwajima…mshenga alikuwa Gwajima wa Edward Lowassa…."

Pia, Soma:

Lissu: Dr. Slaa ndiye alimleta Lowassa CHADEMA
 
17 January 2025
Odero Charles Odero aibuka kidedea katika mdahalo dhidi ya Tundu Antipas Lissu


View: https://m.youtube.com/watch?v=FfS5cmy-nSk

Mwanachama mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Odero Charles Odero leo alikabiliana vikali kwa hoja dhidi ya kiongozi wa juu wa CHADEMA makamu mwenyekiti (bara) Tundu Antipas Lissu.

Odero Charles Odero alihoji staili ya uongozi wa sasa wa CHADEMA ambao Tundu Lissu ni miongoni mwao...

Pia maswali kutoka nchi nzima yalimiminika studio katika kipindi mdahalo ulioongozwa na Chief Odema ambapo ni wagombea wawili tu kati ya wanne yaani Odero Charles Odero na Tundu Lissu ndio walijitokeza leo katika mdahalo ... mwenyekiti Freeman Mbowe na mwanachama Romanus Romanus Mapunda hawakuweza kujitojeza.
 
1737144002431.jpg
 
1737145133788.jpeg

Romanus Romanus Mapunda mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA

Tarehe 19 Desemba 2024 Romanus Romanus Mapunda alifika Makao Makuu ya Chama yaliyopo Mikocheni Dar Es Salaam Tanzania kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa Chama ngazi ya Taifa CHADEMA kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa Chama Mhe. John John Mnyika
 
TOKA Maktaba :

15 January 2025


1737145598612.jpeg


Odero Charles Odero endapo akifanikiwa kuwa Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), amesema atafanya mabadiliko ya mchakato wa uchaguzi wa nafasi hiyo na kwenda mikononi mwa wanachama kuanzia ngazi za mashina.Odero amezungumza hayo leo, alipofanya mahojiano maalum na #MorningTrumpet kuelekea Uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa
 
Back
Top Bottom