Kuelekea 2025 Tundu Lissu arejea nchini, asema atagombea urais 2025 kuitikia wito wa Watanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,229
4,554
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amesema nia yake ya kugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 iko palepale.

Tundu Lissu ameyasema hayo leo, Julai 26, 2024 katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam alipowasili akitokea nchini Ubelgiji.


Tundu Lissu amesema wakati anamkabili Hayati Magufuli alikuwa na umri wa miaka 52, mwaka kesho atakuwa na umri wa miaka 57 hivyo hawezi kuwa na nguvu zile zile za miaka 52 na kwa miaka 57. Lissu meongeza kuwa nguvu ya hoja, na msimamo wa kisiasa na uaminifu kwa watanzania bado uko palepale.

Huyu mama, kama tuliweza kumkabili Magufuli hajatoa matokeo ya urais mpaka leo, huyu aliyekuwa anaua watu, kama tuliweza kumkabilia miaka mitano iliyopita, huyu mama hatakuwa na shida kubwa kama Magufuli.

Pamoja na yote, hii mama mama mama hii ni ya watu waliohongwa na hii haina shida.

Nia yangu ya kugombea Urais iko palepale, nitaitikia wito wa watanzania, nitaitikia wito wa chama changu.
 
Ametangaza jambo hilo alipoulizwa na Mwandishi wa habari iwapo bado anayo dhamira ya kufanya hivyo.

Lissu anesema kwamba Japo 2025 atakuwa na Umri wa miaka 57 lakini bado anaamini atakuwa na uwezo huo.

Screenshot_2024-07-26-18-27-57-1.png
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundi Lissu amesema nia yake ya kugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 iko palepale.T undu Lissu ameyasema hayo leo, Julai 26, 2024 katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam alipowasili akitokea nchini Ubelgiji.
Hachoki
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundi Lissu amesema nia yake ya kugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 iko palepale.T undu Lissu ameyasema hayo leo, Julai 26, 2024 katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam alipowasili akitokea nchini Ubelgiji.
Mbona huwa anasema bila Katiba Mpya hawashiriki uchaguzi? Au kabadili gia?
 
Back
Top Bottom