Huyu jamaa anaanza kuchanganyikiwa sasa.
Tunda Man toka jana mwezi wa 8 alikuwa anatangaza Kuwa mashabiki wake wajiandae na ngoma yake mpya inaitwa "Mwanaume suruali" akaweka mpaka Post Instagram anakumbuka ile.
Huo wimbo hakutoa tena akaja kutoka wimbo mwingine wa kuitwa "Debe Tupu" kwenye interview zake akaja kusema kuwa MwanaFA alimpigia simu na kumuomba abadili jina la wimbo wake ili wasiwachangaye mashabiki.
Na ndio kitu ambacho Tunda alifanya akabadili jina la wimbo wake kutoka "Mwanaume Suruali" mpaka "Debe Tupu".
ukiusikiliza Debe Tupu na Dume suruali ni nyimbo mbili zenye maneno,ujumbe na mahadhi tofauti...Ninachokiona jamaa anajaribu kutafuta Kiki baada ya wimbo wake kubuma.