Tunawezaje kutofautisha kati Uislamu, Ukristo na Uyahudi?

alitosis

Senior Member
Apr 30, 2017
107
64
Uislam, Ukristo na Uyahudi ni dini za Kiabrahama zinahusisha imani za kidini ambazo zinatokana na urithi wa kiroho wa Nabii Ibrahim (Abraham), ambaye anachukuliwa kuwa baba wa imani hizo.

1. Uislamu: Imani ya kwamba kuna Mungu mmoja (Allah), na Nabii Muhammad ndiye mjumbe wake wa mwisho. Ibrahim anaheshimiwa sana kama nabii wa Mungu na mfano wa utii.

2. Ukristo: Wakristo wanaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na Mwokozi. Ibrahim anachukuliwa kama mfano wa imani, na kizazi chake kinachofungamana na ahadi za Mungu.

3. Uyahudi: Unahusisha imani kwamba kuna Mungu mmoja ambaye alifanya agano na Ibrahim na kumwahidi ardhi kwa kizazi chake. Wana wa Israeli wanachukuliwa kuwa warithi wa ahadi hii.

Dini hizi zinashiriki misingi ya pamoja kama vile imani ya Mungu mmoja, maandiko matakatifu, na hadithi za manabii kama Ibrahim, lakini zinatofautiana katika mafundisho, ibada, na uelewa wa majukumu ya manabii na mwokozi.
 
TOFAUTI YA HIZO DINI TATU NI STATUS YA YESU. YESU NDIO KIINI CHA MIGOGORO YA WATATU HAO.

waislam wanaamini Yesu ni mtu, alikufa akazikwa. Alikuwa na kipaji cha kuwa nabii. Akaandika kitabu kinachoitwa injili ambacho hata wao hawajui kilipo.

Wakristo wanaamini Yesu ni Mungu, aliacha utukufu wa uungu akafanyika mwanadamu ili awaokoe watu, akafa, akafufuka yuko mbinguni, hai mwenye sifa ya uungu 100%.

Wayahudi hawaamini kama Yesu alishawahi kuja. Akija atakuja kama mfalme wa kisiasa. Aliyekuja wao wanamuona ni mzushi tu aliyepotosha vijana wale 12 na wafuasi wao.
 
Uislam,Ukristo na Uyahudi ni dini za Kiabrahama zinahusisha imani za kidini ambazo zinatokana na urithi wa kiroho wa Nabii Ibrahim (Abraham), ambaye anachukuliwa kuwa baba wa imani hizo.

1. Uislamu: Imani ya kwamba kuna Mungu mmoja (Allah), na Nabii Muhammad ndiye mjumbe wake wa mwisho. Ibrahim anaheshimiwa sana kama nabii wa Mungu na mfano wa utii.

2. Ukristo: Wakristo wanaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na Mwokozi. Ibrahim anachukuliwa kama mfano wa imani, na kizazi chake kinachofungamana na ahadi za Mungu.

3. Uyahudi: Unahusisha imani kwamba kuna Mungu mmoja ambaye alifanya agano na Ibrahim na kumwahidi ardhi kwa kizazi chake. Wana wa Israeli wanachukuliwa kuwa warithi wa ahadi hii.

Dini hizi zinashiriki misingi ya pamoja kama vile imani ya Mungu mmoja, maandiko matakatifu, na hadithi za manabii kama Ibrahim, lakini zinatofautiana katika mafundisho, ibada, na uelewa wa majukumu ya manabii na mwokozi.

"Kwani tunataka kutambika?" --- JKN
 
. Hivyo ni vitabu tu vilivyoandikwa na WAHUNI HAPA DUNIANI, sidhani kama Vina uhusiano wowote na uwepo wa mungu.

. Mtu wa DINI anakuambia Ukifa unaenda kwa MUNGU, Lakini huyo Mtu huyo huyo wa Dini anaogopa kifo 🥴🥴🥴
 
TOFAUTI YA HIZO DINI TATU NI STATUS YA YESU. YESU NDIO KIINI CHA MIGOGORO YA WATATU HAO.

waislam wanaamini Yesu ni mtu, alikufa akazikwa. Alikuwa na kipaji cha kuwa nabii. Akaandika kitabu kinachoitwa injili ambacho hata wao hawajui kilipo.

Wakristo wanaamini Yesu ni Mungu, aliacha utukufu wa uungu akafanyika mwanadamu ili awaokoe watu, akafa, akafufuka yuko mbinguni, hai mwenye sifa ya uungu 100%.

Wayahudi hawaamini kama Yesu alishawahi kuja. Akija atakuja kama mfalme wa kisiasa. Aliyekuja wao wanamuona ni mzushi tu aliyepotosha vijana wale 10 na wafuasi wao.
Waislam hawaamini kuwa Yesu alikufa,though hawana andiko linalosema hivyo, lakini wana Amani Yesu hakufa.

kuhusu ukristo:, YESU NI MWANA WA MUNGU,SIO MUNGU.
 
TOFAUTI NDIO HII;

Yesu akajibu akamwambia: “Mimi ndiye njia na kweli na uzima. Mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya Mimi"
YOHANA 14.6
 
Waislamu wanaamini vitabu vinne ambavyo ni 1. Tarurati, Zaburi, Injili na Quran

Wakristo wanaamini vitabu 3 yaani Taurati, Zaburi na Injili

Wayahudi waanaamini Vitabu viwili tu yani Taurati na Zaburi

Hivo hivo upande wa Mitume, waislamu wanaamini Mitume wote kuanzia Adam mpaka Muhammad SAW, Wakristo wao wameishia kwa Isa (Yesu) Muhammad SAW hawamuamini, na Wayahudi wao walikataa kuwaamini baadhi ya Mitume kama Zakariya, Yahaya (Yohana) Issa (Yesu) na Muhammad SAW

Ukitaka kuujua ukweli wa hizi dini fanya juhudi ya kusoma vitabu hivi vyote bila kubagua hata kimoja, na kisha utaona mwenyewe kwa macho yako tofauti na utajua kweli ni ipi na uongo ni ipi.

QURAN katika Surah Baqara, Al-imran, Al-Maida, na Al-aaraf imeelezea vizuri tofauti kati ya hizi dini tatu na nani kakosea wapi.. so for your knowledge read the Quran will help you understand

QURAN ya kiswahili ipo hata online unaweza kusoma. Mwenyezi Mungu atuongoze katika njia ya kweli. Amina
 
Kwa upande wa ukristo hautambui uwepo wa uislam labda kama uislam umetajwa kwa jina jingine katika unabii kuwa utatokea. Dini ya kiyahudi imekuwepo tangu zama na zama Yesu aliikuta na akaiacha. katika mji wa antiokia ndipo ukristo ulipoanza na waumini wake wanaitwa wakristo, yaani wafuasi wa mafundisho ya Yesu Kristo
 
Quran imetaja hizi dini zote kwa majina yake na kuelezea tofauti zao, Kumbuka Quran ndio Kitabu cha mwisho kilicholetwa miaka 600 baada ya Injili kwa hivyo Mwenyezi Mungu ameelezea vizuri vitabu vilivyopita kwa undani hasa. Sio lazima uwe muislamu ndio usome Quran but unaweza kusoma tu kwa uelewa wa dini hizi tatu
 
Umesahau kutaja hadithi kibao ambazo Waislamu huziamini hata kuliko Kurani yenyewe. Ni sawa na Wakatoliki wanaoamini mapokeo kuliko hata Biblia yenyewe.

Naweza kusema kwamba hivi sasa kuna Ufarisayo na Usadukayo mwingi mno kwenye Uislamu, kama ulivyokuwepo Ufarisayo na Usadukayo wakati Yesu akiwepo duniani.
 
Back
Top Bottom