Tunatafuta huruma kisiasa au ndio ajenda mpya

mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
663
1,165
Nacheka suala la kisheria linavyopewa sura ya kisiasa.

Kuna mambo hayahitaji kulazimisha bali kuyaelewa tu.

Kupeleka ushahidi mahakamani haitoshi kumtia hatiani mtuhumiwa. Sijui kwa nini watu wanaiogopa Vodacom inapotekeleza takwa la kisheria.

Iliwahi kutokea
:

Kuna Dada mmoja alikuwa anafanya kwenye Biashara ya M-PESA, Tigo-Pesa, AirtelMoney, Fahari Huduma, Maximalipo, mtaji wa Biashara hiyo ulikuwa 20 milioni.

Dada akatoweka ghafla na akaacha vitendea kazi vyote mashine na simu ila having salio, amepakuwa lote.

Kesi ikaenda polisi, utaratibu wa kumtrace mtuhumiwa ukafanyika, ushahidi ukakusanywa na watu wawili wakatiwa mbaroni akiwemo yule Dada na mwanaume mmoja.

Kesi ikafika mahakamani.

Dada alikuwa anatumia simu binafsi ya mtandao wa Tigo, mawasiliano yake yalipochunguzwa kuna mambo yalibainika.

Tigo walikuwa mashahidi wa mlalamikaji kuieleza mahakama mawasiliano ya mtuhumiwa na mwanamume ambaye nae ni mshtakiwa namba mbili.

Kuna mambo yalibainika kutoka ushahidi wa Afisa wa Tigo alioutoa mahakamani._

Kumbe yule jamaa wa mjini alijifanya mteja wa yule Dada wakazoeana, akamtongoza, akamuahidi Ndoa. Kisha kupitia sms-chats wakaongea mengi Dada akamtajia na kiasi cha mtaji wa ile biashara, jamaa akampa mchongo Dada atoe ule mzigo wote kisha wasepe zao wakaoane waanze maisha. Dada akakubali mpango, akafanya yake wakabeba mzigo wakapotea.

Mahakama ilishawishika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani na ikawatia hatiani watuhumiwa wote wawili na kuwahukumu kifungo gerezani pamoja na kulipa ile 20milioni ya mlalamikaji vyote kwa pamoja.

Hivyo, sio mara ya kwanza kwa haya makampuni kutoa ushahidi pale wanapotakiwa kufanya hivyo kisheria.

Hili la Lema sio la kwanza na halitakuwa la mwisho.

Tuiache sheria ifuate mkondo wake.

Mahakama ndio itaamua kukubali au kuukataa ushahidi.

Kuligeuza jambo hili ajenda ya kisiasa ili kutafuta huruma ya jamii tunapotoka na kupotosha wengine.

Tuwaache Voda watekeleze matakwa ya sheria. Tuiache mahakama iamue kwa uhuru na haki.
 
Sijawahi sikia mtu kapona kwenye ushahidi wa kimtandao. Maana hausemi uongo, hata kwenye uzi wako umethibitisha. Cha msingi hapa kuwahi kwa mganga. Im kidding.
 
Hakuna MTU aliyewakataza tumesema tunaanza na Vodacom period.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…