Tunapoelekea mwaka mpya 2025, nashauri nyote kutumia Condom wakati wa kujamiina tumalize mwaka na afya njema

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
19,947
21,963
Lengo la ushauri huu ni kuvuka mwaka bila kua na UTI sugu, gono, kaswende au UKIMWI ambao umenusurika nao kwa sehemu kubwa sana ya mwaka huu2024, na mwaka wenyewe unaelekea kuisha hivi karibuni.

Huna haja ya kunishukuru, ni muhimu sana kumshukuru Mungu kwa kila jambo kwa mwaka mzima2024.

Aidha nawashukuru sana wadau wote wa jukwaa hili muhimu la MMU, kwa namna ambavyo tumeelimishana, tumeonyana, tumejuzana na kufahamishana mambo mbalilimbali kuhusu mahusiano, urafiki, uchumba na ndoa, lakini pia visa na mikasa ya huzuni na furaha katika mapenzi n.k.

Binafsi kama kiongozi,
nimenufaika pakubwa kuchangamana na kufurahi nanyi marafiki na waTanzania wenzangu kwa mwaka mzima2024.

Kwa kuhitimisha nawatakia nyote maandalizi mema sana ya likizo za sherehe ya Chrismass na ile ya mwaka mpya 2025.

Neema na Baraka za Mungu ziambatane na kuanadamana nanyi nyote, katika kazi na majukumu yenu ya kila siku daima na milele.

Aimen :pulpTRAVOLTA:
 
Back
Top Bottom