Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,051
Hukumu ya kihistoria imetolewa katika mahakama za huko America, Kwa Rais mstaafu wa nchi hiyo, Donald Trump, kukutwa na hatia Kwa makosa 34 ya jinai, aliyoshitakiwa nayo.
Hiyo inamfanya Donald Trump, kuwa Rais wa kwanza mstaafu wa America, kukutwa na hatia, Kwa makosa ya jinai tokea Taifa Hilo liundwe.
Kwa nchi yetu najua Hilo haliwezekaniki kutokea, Kwa kuwa Taifa letu, watawala wetu wametengeneza Katiba, inayompa Kinga Rais yeyote anayedumu Kwenye madaraka, kuwa hatashitakiwa Kwa makosa yoyote, anapokuwa madarakani na hata pale anapostaafu!
Ndiyo maana madai yanayotolewa na wananchi walio wengi, pamoja na vyama vya upinzani vya nchi hii ya madai ya kuandikwa upya wa Katiba ya nchi yanakuwa na nguvu, ingawa yanapingwa sana na viongozi wa serikali hii ya CCM.
Swali hapa ni kuwa kama nchi tunapata fundisho gani Kwa Rais mstaafu wa Taifa kubwa na lenye nguvu kubwa za kiuchumi, kukutwa na hatia Kwa makosa ya jinai aliyoyafanya akiwa madarakani?
Somo pekee tunalopata hapa ni kuwa hakuna Binadamu, aliye juu ya Sheria, hata Rais wa nchi anapaswa kushitakiwa, iwapo atafanya makosa ya jinai.