Tunaomba Serikali iingilie Kati hili la soko la TAZARA Tunduma ili kunusuru uchumi wa wanainchi wa tunduma

Killing machine

JF-Expert Member
Jul 24, 2022
1,989
2,906
Nikiwa kwenye mizunguko yangu ya kibiashara mkoani songwe nimekutana na Jambo ambalo limeni shangaza kidogo Kama sio Sana

Tunduma Kuna soko lakimataifa la mazao linaitwa mataifani

soko hili Lina patikana km.5 kutoka ulipo mpaka wa Tanzania na Zambia

Lakini Tena kunasoko lingine la mazao lipo mpakani mwa tanzania na Zambia linalo itwa tazara

Linaitwa tazara kwasababu lipo ndani ya kata ya tazara iliyopo upande wa Tanzania

Soko hili lipo kalibu kabisa na Zambia ukiwa kwenye soko hili unaweza kuziona beacons za mpaka wa Tanzania na Zambia

Sasa soko hili nisoko ambalo lipo hapo toka enzi na enzi za mababu zetu nisoko ambalo Lina waunganisha wazambia na watanzania

Ukizingatia Kuna kabila linaitwa wanya mwanga ambao Hawa wapo pande zote za inchi zote mbili

Yani kwa upande wa Tanzania Wana patikana tunduma na kwa upande wa Zambia wanapatikana nakonde

lakini wote Hawa Wana ongozwa na chief mmoja aliyepo zambia Ana itwa chief naitwika Kama sjakosea

Sasa Kama inavyo julikana kwamba wazambia niwakulima wazuli wa ulezi,mahindi,karanga,soya beans nk

Wavunapo mazao haya huja kwenye soko Hilo Kuja kuyauza mazao yao hivyo hivyo kwa kipindi Kama hiki au msimu huu ambao wenzetu wazambia

Hawakupata mvua za kutosha wazambia huja kununua mazao kutoka Zambia kwenye soko Hilo Lili lipo mpakani mwa Tanzania na Zambia kwa ajiri ya chakula na biashara

Kiukweli soko Hilo Ni soko kubwa mno kwani nimeshuhudia wafanya biashara mbali mbali kutoka Kenya,sudani,somaria,Zim abwe,Congo nk

Wakija sokoni hapo Kuja kununua mazao mbali mbali Kama soya beans,karanga,ulezi,Michele nk

Nisoko ambalo naweza kusema limeshikilia mzunguko mzima wa pesa za mji mdogo wa tunduma kwamfano ifikapo miezi ya mavuno/kiangazi

Kuna wakati banks za tunduma huishiwa pesa"

najua huwezi niamini lakini ipo hivi.

Kwa mfano kg.1 ya soya beans Ni shilling 1900 Mara Mia moja sawa na 190000 Mara 30 tones inakuja 57000000 millions

Sasa kwa siku mzigo unao ingia wa soya sokoni hapo kwa siku kwa kipindi Cha kiangazi Ni zaidi ya gari 20 sasa tufanye Kama Ni gari 20 za 30 tones

Naomba uschoke kusoma mkuu wangu

sasa piga 57000000 times 20 utapata idadi ya pesa inayo enda kutolewa kwenye banks zetu kwa siku

Hapo bado Kuna pesa zina tolewa kwa ajili ya kununulia ulezi,mahindi,karanga, nk

baada ya pesa hizo kutolewa Kuna vijana wamejiajili kwenye ununuzi na uuzaji wa kwacha huenda kuichenji hizo shillings kwenda kwenye kwacha

Na kuwalipa wateja wao wazambia walio Kuja na mizigo hiyo hivyo kupata japo mkate wa Kila siku kupitia kazi hiyo

Lakini pia Kuna watu waserikali huja kuchukua ushuru wa soko na maegesho

Kuna wasafirishaji wa mizigo Kuna akina mama lishe,Kuna wafanya biashara wa vyumba vya kulala,lakini pia Kuna vijana walio jiajili kwenye kushusha kupima na kupakia,bodaboda nk

Wote hawa wanalitegemea soko Hilo la tazara

Chakushangaza
Kuna watu wachache walio Jenga vyumba/flames kwenye soko la kimataifa

Ili kuhakikisha vyumba vyao vina pangishwa na wafanya biashara wa mazao watu hao kwakutumia madaraka yao ya uchama

wameamua kwa makusudi kulihujumu soko Hilo kwa kulazimisha soko Hilo lifungwe na libaki soko la kimataifa pekee

Watu Hawa wengi wao nivi gogo wa ccm pale tunduma wanatumia ushawishi wa chama kuuwa ajira kwa watu zaidi ya 2000 waliopo ndani ya soko la tazara

Lengo likiwa nimoja tu wafanya biashara na madarali wa soko latazara wahamie mataifani wakapange na kutumia vyumba walivyo vijenga wao

Mpaka sasa soya,ulezi,karanga vina zuiwa visiingie Tanzania kutoka Zambia

Lakini pia mahindi haya ruhusiwi kwenda sokoni pale isipo kuwa soko la kimataifa

Biashara zime simama tunduma banks hazifanyi kazi Kama mwazo naweza kusema nikipindi kigumu mno kwa wafanya biashara wa tunduma

Na kibayaha zaidi serikali imeingia hasara kwa kujenga soko kubwa kwa ajili ya biashara hapo tazara ikiwemo Barbara ya lami kutokea Kilimanjaro mpaka tazara

Sasa najiuliza kulikuwa Kuna haja gani ya kujenga barabara Tena ya kiwango Cha lami na wakati huo huo wakasitisha magari kupitisha mizigo kwenda sokoni hapo?

Je!kulikuwa na haja gani ya kujenga soko lenye kiwango kile huku wakijua lile sio soko?

Je! wanatuma watu waushuru wanini huku wakijua lile sio soko?

Je! Ni ipi hatima ya vijana,boda,wasafirishaji,mama lishe,na wapiga kula wengine walio kuwa Wana pata liziki zao na kulipa ushuru wa inchi kupitia lile soko?

Je! Kama inchi haioni hasara kupoteza ushuru mkubwa kiasi hicho uliokuwa unaingia kupitia soko hilo?

Mwisho ningeshauri harmashauri husika kukaa na kufikiria kuhusu faida na hasara za kulizuia soko hilo kabla

Badara ya kuamua kwa kushinikizwa na watu wachache wenye masrahi yao binafsi
 
Back
Top Bottom