Nimeshuka kwenye basi la haraka kituo cha Ubungo terminal napita darajani nivuke barabara naona jamaa wananidai pesa.
Nikawabia mimi sisafiri navuka barabara hawataki. Ikabidi nitudi nyuma,je mh Makonda kupita kwenye hili daraja tunalipia?
siyo mateja ni wale wahudumu sijui wakata ushuru pale getini, yaani wanavyodai hizo pesa utafikiri ni za kwao.Hao ni mateja tu; Makonda atupie macho hapo.
siyo mateja ni wale wahudumu sijui wakata ushuru pale getini, yaani wanavyodai hizo pesa utafikiri ni za kwao.
kuna siku nilikuwa nasafirisha mzigo na nilikua nakimbizana na muda, nimefika pale nina 10000 tu nikawapatia wanasema nafanya kusudi hivyo nibakie nisubiri,
niligombana nao mnoo uzuri nilikua na jezi ya mule ndani nikatumia ubabe kuingia,
Pale panahitajika mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato,
na sijui ni kwa nini wanalipisha mtu kuingia katika kituo cha mabasi???.
Wapumbavu sana. Next shika hata kipande cha gazeti mkononi mkuu utapita kirahisi tu.Leo nimelipa 200 kupanda Daraja la UDART kupitia Ubungo Bus Terminal. Vijana getini wamenizonga wakinilazimisha kulipa 200 kwa kuwa nimekanyaga Ubt. Eti watajuaje usafiri wa mikoani na wa UDART? Nikaenda tena kulipa 650 kwenda mjini. Jumla 850
Ni halali kulipa Geti la Ubungo ilihali sisafiri? Vijana mwenyewe Wa getini washari kweli.
Kama wamekupatia risiti ni sawa
Sio kila mtu anatokea upande wa depot. Kumbuka lile daraja lilijengwa kuvusha watu. Sasa mimi sielewi wanashindiwa nini kukusanyia hizo 200 zao kule ndani ili kutenganisha anayeenda UBT na UDART. Jambo doooogo lkn lazima watu washikane mashati ndio kazi ifanyike.ukipandia upande wa depot ya tbl hakuna charge yeyote mkuu.
Natokea Chuo kikuu, nikashuka kwenye foleni darajani. Hivyo ikabidi nitembee kupita hao vijana wasumbufu wanaokera abiria wa Mikoani. Upande huo kuna Daraja sikutaka kuvuka barabara hatarishi za mwendo kasi. Wanaolipisha ushuru kwenye mageti ya Vumbi walinizonga sana wakidai no way bila 200. Polisi wako mbali ningewaomba msaada.hukuweza kupandia upande wa TBL depot?
uko sahihi.Sio kila mtu anatokea upande wa depot. Kumbuka lile daraja lilijengwa kuvusha watu. Sasa mimi sielewi wanashindiwa nini kukusanyia hizo 200 zao kule ndani ili kutenganisha anayeenda UBT na UDART. Jambo doooogo lkn lazima watu washikane mashati ndio kazi ifanyike.