Baada ya kukosa hoja za msingi kuhusu utendaji wa Serikali, na baada ya kuona kwamba tumeachana na Sera yetu ya Ufisadi iliyotubeba nyakati zile na kutupatia umaarufu, TUMEJIULIZA TUTATOKAJE?
Tumepata jibu kwamba angalau basi wananchi watuone tukizomea na kupiga kelele kama siku ya uzinduzi wa Bunge kwa kuimba kama vyura" Maalim Seif, Maalim Seif, Maalim Seif na hatimaye kutoka ndani ya Bunge. Tukaja kudai kujadili hotuba ya Mheshimiwa Rais "live" ingawa hatukuishuhudia Bungeni maana tulikimbilia Mnadani kula nyama siku ile!
Hawa Serikali mbona wanatubania sana sisi na sasa hatusikiki kabisa?? Au wamedhamiria wananchi watusahau kwa porojo zetu za kupinga hata Ukweli? Ndio maana sasa tunalianzisha kwa kutetea Majipu kwa kisingizio cha haki za Binadamu!! Kutetea Watumishi wazembe kwa kisingizio cha Sheria na taratibu kuzingatiwa, kutetea wakwepa kodi kwa kisingizio cha kwamba wanaoonewa ni wanachama wetu!! ACHA TULIANZISHE MAANA HATUNA UMAARUFU TENA!! PIPOOOOOZ! PAWAAAAAAAAAAAAAA!!