Tunajazwa upepo, Makusanyo ya TRA ya Magufuli ni sawa na ya TRA ya Kikwete

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Tumeaminishwa makusanyo kwa mwezi ni zaidi ya Trilion 1.3 kwa mwezi serikali iliyopita walikuwa wakikusanya chini ya Bil 900. Tukashangilia lakini ukiangalia kwa makini thamani ya shilling zidi ya dolla unakuta hakuna tofauti ya ukusanyaji kodi kwa serikali hizi.

Haya ukiangalia kwenye "inflation" yaani kupanda kwa gharama za maisha kutokana na ongezeko la fedha ama lugha nyingine mfumuko wa bei unagundua hakuna ongezeko. Tunalishana upepo na deni la Taifa linazidi kupaa. Napongeza juhudi za kukusanya kodi ila ningetegemea kuwe na unafuu basi kwa mtanzania masikini.

Ongezeko kwenye kodi ya kila bidhaa pamoja na miamala ya kibenki na mitandao ya simu ni mzigo kwa masikini manufaa ya kukusanya zaidi ni hadithi ya kulishana upepo.
 
acha kuaibisha jf, kwani hiyo kodi ilikuwa inakusanywa kwa dola wakati useme rate imebadilika sasa hivi,

kama ulikuwa unalipwa mshahara 10,000 mwaka jana, alafu bosi akakuongezea ikawa 15,000 unaweza kusema exchange rate ndio imebadil huo mshahara,
 
Usingekurupuka alafu ukaja kwa mwendokasi basi ungenielewa
 
Wewe uta anzisha nyuzi mwaka huu hadi utachanganyikiwa!
 
umenena kweli mkuu. ila tofauti tu ni kuwa labda kwa sasa hawataiba zote kwi-kwi-kwi!
 
Mtoa mada vipi???? hoja ni ipi? kodi hisikusanywe, au kodi haikusanywi, wananchi wasilipe kodi??? hoja ni nini? unatoa upepo tu, hujaandika kitu, unaonesha hisia tu, husiwe mlopokaji kama Lissu, itakugharimu
 
Nani anawajali hao masikini?
 
acha kuaibisha jf, kwani hiyo kodi ilikuwa inakusanywa kwa dola wakati useme rate imebadilika sasa hivi,

kama ulikuwa unalipwa mshahara 10,000 mwaka jana, alafu bosi akakuongezea ikawa 15,000 unaweza kusema exchange rate ndio imebadil huo mshahara,
Zimbabwe kio moja ya sukari ni sh 400,000
 
Kwa hiyo TRA wanakusanya US $ harafu wana convert to madafu? Impact ya devaluation tuwaachie watalaam.
 
Mtoa mada vipi???? hoja ni ipi? kodi hisikusanywe, au kodi haikusanywi, wananchi wasilipe kodi??? hoja ni nini? unatoa upepo tu, hujaandika kitu, unaonesha hisia tu, husiwe mlopokaji kama Lissu, itakugharimu
Wewe ndi huna ulicho kiandika jaribu kupitia kusoma utagundua kuwa umeandika pumba tupu
 
Mbona umeandika bila facts? umeandika kijuu-juu saaana sa sijui tunajadili nini hapa?

tunaomba jumla ya makusanyo uliyonayo yanayothibitisha madai yako,

Makusanyo ya TRA ni kwa TSHS. siyo kwa $

Inflation inategemeana na uzalishaji au upatikanaji wa bidhaa au huduma husika, sasa hii inahusika vipi na makusanyo ya kodi ya TRA?

Thamani ya dola dhidi ya Tshs. Magufuli ameikuta hvyo toka kwa JK. kwa sasa ndo anapambana kuipa thamani Shilingi yetu na ili kuipa thamani sh. yetu kuna mambo mengi ya kufanya.

Hakuna ongezeko la kodi kwenye kila bidhaa ni baadhi ya bidhaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…