Watanzania 7 kupeperusha Bendera ya Tanzania katika Olimpiki 2024 huko Paris

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,085
1,767
IMG_2583.jpeg


UPDATE: Tangu kuanza Kushiriki Olympics (1964), Tanzania ilipata Medali 2 tu za Fedha (Silver) kupitia Filbert Bayi na Suleiman Nyambui huko Moscow (1980). Leo Julai 29, 2024, Mcheza Judo Andrew Mlugu leo anatafuta Medali ya 3 akikabiliana na Joan-Benjamin Gaba (23) wa Ufaransa​

Mlugu (28) anashiriki raundi ya 16 ya mashindano ya Kilo 73 (Super Middle Weight) katika Uwanja wa Champs-De-Mars


Timu ya Tanzania itawakilishwa na Wanamichezo 7 katika Michezo Mitatu, (Judo, Riadha na Kuogelea)

Katika Riadha, Watashiriki wanariadha 4 wa mbio ndefu, Wanaume 2 (Alphonce Felix Simbu na Gabriel Geay) na Wanawake 2 (Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri)

Judo, Mshiriki 1 (Andrew Thomas Mlugu) na Waogeleaji 2, Sophia Anisa Latiff (Mita 50 freestyle) na Collins Phillip Saliboko (Mita 100 freestyle)

Kuanzia leo Julai 26, 2024 Wanamichezo bora Duniani zaidi ya 10,000 wanajumuika Nchini Ufaransa, Jijini Paris katika ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Olimpiki, ambapo Medani 300 tuu za Dhahabu zinashindaniwa

Wanamichezo watashindana kukimbia, kuruka, kuogelea, judo, ndondi, tenisi, polo, golf, kuendesha Baiskeli, kuendesha Mashua, mazoezi ya Viungo na mingine mingi

Sherehe ya ufunguzi inafanyika leo Julai 26, 2024, huku kukiwa na jumla ya siku 19 za mashindano. Medali ya kwanza ya dhahabu itashindaniwa kesho Julai 27 na itakuwa kutoka kwenye mashindano ya kupiga risasi.


Sherehe ya kufunga Mashindano itafanyika Jumapili, Agosti 11, 2024

Unadhani Timu ya Tanzania italeta Medali ngapi nyumbani?

.........

This year, the world's greatest athletes will come together in France's capital city Paris to run, jump, swim, twist, twirl, kick, punch and climb their way to the top of the Olympic podium.

These Games are, for many athletes, the pinnacle of their sport - there is no greater achievement than earning an Olympic gold medal.
But with more than 10,000 athletes competing and only 300 gold medals up for grabs, only the best will be able to call themselves Olympic champions when the Games end.

So, here is everything you need to know about the 2024 Olympics.

When do the Paris Olympic Games start?

What a spot for an Olympic selfie!
The opening ceremony will take place on Friday 26 July 2024.
There will be a total of 19 days of competition but some preliminary events take place before the opening ceremony, such as archery qualifying and early rounds of rugby sevens, football and handball.
The first gold medal will be won on Saturday 27 July and will likely come from the shooting ranges, with rifle and pistol shooting competitions kicking things off.

This will be followed by 16 days of world class sport, and Newsround will be in Paris to make sure you don't miss a moment.
The closing ceremony takes place on Sunday 11 August.

What sports will we see at the Paris Olympics?

Team GB's Charlotte Worthington took gold in Tokyo - can she do it again in Paris?

There will be plenty of the traditional Olympic sports such as athletics, swimming, rowing and cycling as well as gymnastics, badminton, tennis and boxing.

This year, surfing, skateboarding, BMX freestyle and sport climbing will also return after their success in Tokyo.


There will also be the brand new addition of breaking at this year's Games, which is a form of acrobatic dance where competitors combine power moves and freezes to impress judges and earn themselves the Olympic gold medal.

We can also expect to see combat sports such as taekwondo, judo and wrestling.


The Olympics is often a great opportunity to see sports you don't get the chance to watch very often, for example water polo, artistic swimming, fencing, handball and basketball.

New events in the sailing competitions will also include a form of windsurfing called iQFoil and kiteboarding.


Sources: CNN, BBC Sports, Reutters
 
Jamaa wanaweza sana wameandaa nje ya uwanja katikati ya jiji la paris karibu na mnara wa Notre Dame

Washiriki wa nchi mbalimbali wamepita juu ya mto wa maji wakiwa kwenye boti za wazi wakionesha bendera za nchi zao

Ufunguzi huu upo supa sana namuomba zinedine zidane akimkimbiza mwenge wa olimpiki

More updates to come

USSR
 
TV Station gani ya Bongo wanaonyesha?, mpira wa miguu Africa nchi gani zinatuwalisha?.
 
Wacheza Tennis wametalawa kwenye kubeba mwenge wa Olympic... Yupo Nadal na Serina Williams... Football namwona Zidane... Kwenye riadha Carl Lewis...

Ufunguzi huu umenoga sana... licha ya kimvua
 
Mwenge umebebwa na watu wengi... Mmojawapo ni Mfaransa aliyeshinda medali miaka 1940... Sasa ana umri wa miaka 100
 
Hitimisho la mbio ya mwenge wa Olympic ni kuwasha ama kurusha hot air balloon.....kama ishara ya ufunguzi rasmi wa michezo ya Olympic.....
 
Kilichofurahisha ni kumwona Celine Dion akirudi kwenye live performance katika ufunguzi huu wa Olympic
 
Nakumbuka nani atavunja rekodi ya mwamba wa jamaica mita 100 range ya urefu wa mpira wa miguu kwa sekundi 9 usain bolt jamaa ni hatari
 
Salam wadau,
Binafsi kwa namna moja au nyingine nimekua nikifuatilia updates kuelekea mashindano ya olympics huko Paris-Ufarasa.

Kwa kuanzia nimeona namna ambavyo team mbalimbali kutoka nchi tofauti tofauti zimeandaa vazi maalum kwaajili ya mashindano haya ambapo nchi za Haiti na Mongolia zimetisha sana. Nimejitahidi kutafuta vazi rasmi la Tz katika mshindano haya lakini nimetoka kapa, jirani zetu (Ke) wameenda na vazi kama la kimasai lakini limekua miyeyusho sana.

Haijaishia hapo hiyo olympic vilage (ambapo ndio makazi ya athlete hao) imekua na features za tofauti kidogo, na hao washindani wamepatiwa vitu mbali mbali ikiwa ni pamoja samsung flod, Shoes kulingana na size yao pia menu yao na vyumba vimekua tofauti sana of which team yetu na nchi kwa ujumla ilikua inakitu cha kujifunza.

Mambo yasiwe mengi, baadhi maswali nnayojiuliza kama ifuatavyo

i) Hivi Bongo tumepeleka team kweli..?

ii) Kama tumepeleka, je ipo well funded na ipo proud kuiwakilisha Nchi au ndio mpaka ipate hype ya media, usikute athletes hawajakabidhiwa hata bendera(full kuunga unga)

iii) Tuliandaa vazi la mashindano (olympic custome) tunaomba lipite kimya kimya

Mambo, maswali ni mengi lakini nahisi kumasehemu kama nchi nawasiwasi tumefeli katika hili jambo ( inakuaje hata uki-google Tanzania 2024 olympic custume natoka bila bila hata timu ya wawakilishi huioni (kubanake) .

Katibuni kwaajili ya kunirekebisha na kunifungua zaidi kama kunataarifa ilinipita juu ya haya mashindano.
 
Back
Top Bottom