Tunaegemea upande gani, ujamaa au uliberali?

P J O

Senior Member
May 3, 2024
101
142
Tanzania 🇹🇿 tunabahati ya kuishi katika Nyakati mbili za mifumo ya utawala, yani katika UJAMAA/Communism na Liberal/Liberali yani kidemocrasia.

Mifumo yote Ina mazuri yake na mabaya Yake. Kua katika mrengo usieleweka pia una athiri nchi kiuchumi katika upande hasi nitaeleza chini.

Kua Liberali Ina maanisha wananchi wanaruhusia kumiliki na kuendesha shughuli zao za kiuchumi including social service Kwa manufaa Yao wenyewe na taifa.

Kwa Tanzania tunajiita UJAMAA na kujitegemea na hii imeathiri sana na kuleta ugumu katika kufungua fikra na fursa Kwa wananchi kumiliki biashara nchi na mwishowe watu kutoka mataifa mengine huja na kutumia fursa kufungua viwanda na biashara kubwa. Mfano mzuri Dar Es Salaam, kuanzia Airport mpaka Kariakoo makampuni/Viwanda vya kitanzania ni vingapi ukilinganisha na foreigners.

Mazingira ya Biashara TANZANIA ni magumu, Kodi ni nyingi na kama wazawa wanashindwa kutengeneza mtaji hata mdogo kuanzisha na kuendesha biashara Kwa uhuru.

Serikali Ina miliki karibu Kila kitu nchini, uendeshwaji wa baadhi ya hizi huduma sio mzuri mfano Idara ya maji, Mashule, hospital, MSD na kadhalika. Na Bado inazidi kujitanua yenyewe, pale inaposhindwa kutekeleza kama kwenye swala la Bandari huwaachia makampuni ya kigeni. Kitu ambacho inadhani inalinda maslahi yake lakini inaua nafasi Kwa wazawa kujijengea uchumi mzuri na kuuza taifa ambalo ni kweli la viwanda.

Kandarasi za ujenzi wa Barabara na majengo makubwa Bado tunategemea china na tunajiita democrasia, Kwa Nini serikali isikodishw mashine Kwa local engineers wajenge barabra zetu wenyewe.

UJAMAA tunaoshikilia unanufaisha makampuni ya nje, na tunaendelea kua tegemezi wa mikopo. Dira ya taifa inabidi iwe Moja na uelekeo mmoja

Paul J Oscar,
0717 345 688
 
Back
Top Bottom