Tumshauri jamaa yangu huyu

Mzee Chapuuka

Member
Apr 21, 2017
97
243
Wakuu salaam
Ni kwamba nina rafiki angu ambae nlisoma nae leo asubuhi kanipigia simu na kuniomba ushauri kwangu na hata Kwa wadau wengine wa huku Jf
Rafiki angu huyu ana mwanamke wake ambae amezaa nae mtoto mmoja Ila now wanaishi mbalimbali japo ni mikoa ya jirani Sana
Mama mtoto wa huyu jamaa ni muajiriwa na huyu jamaa angu ni mpiga mishe Tu wa town bado mambo yake hayajasettle anapata hela ya kula na kulipa bills za maji umeme na kodi ya chumba ingawa hiyo pesa nayo anaipata Kwa kuunga unga sana hivyo inakua ngumu kumuhudumia mtoto ipasavyo na mamake
Sasa inshu ipo hivi jamaa alipigiwa simu na huyo mama mtoto wake na kumwambia aache kazi anayoifanya arudi Kwa mke wake akakae Tu coz mwanamke anaona hakuna hela inayopatikana
Sasa anataka arudi akakae Tu home jamaa bado anawaza aache kazi then akalelewe Tu na mama mtoto wake ,huku aliko anapata hela japo kidogo Sana lakini hasumbuani na mtu kuomba omba hata vocha sasa je akiacha hii kazi inayomwingizia kidogo na kwenda kukaa jobless na kumtegemea mwanamke Kwa kila kitu itakuaje
Ebu tumshauri huyu jamaa
 
mimi naamini huyo rafiki yako ni wewe mwenyewe, ila chakufanya huwezi kabisa hata kupata milion tatu ukafanya biashara maana kwa maisha ya sasa usiwekeze fikra kwenye kuajiriwa sana. ila huyo baby wako nae anakupenda ndio maana anakuonea huruma
 

MKUU,

UNAMAANISHA KABISA-
WATAKA KWENDA KUMTEGEMEA MWANAMKE???!!!

NAKUPA WIKI 3 TU,
UTAKUJA KUSIMULIA KITAKACHOKUKUTA!!!
 
Na yeye ampe sharti huyo mwanamke amwambie kama unataka nije basi niangalizie mtaji nianze biashara tusaidiane.
 
Nenda kaka wala usiogope, maisha Ni kusaidiana. Hakuna ubaya wowote ukipinda maishani mwenzako kukukwamua. Kitu kizuri kakupigia simu mwenyewe uende. Kama umeshindwa kumuhudumia mtoto financially basi kakae angalau umuhudumie kimaadili na kimazingira.

Nenda mjomba
 
Nimekuelewa brother.
Huyo mama anampenda mwenzake na anapenda washirikiane kulea mtoto, ila asikubali kukaa idle bila kujishughulisha. Mwambie kama yuko pouwa financially aanze mishe za biashara ilimradi tu awe anaingiza hata buku kwa siku. Itamsaidia kujenga mahusiano yao lakini kinyume na hapo hawatachelewa kukwazana.
 
Kwani hizo mishe mishe zinazokukeep busy for nothing huwezi kwenda kuzifanya huko aliko baby mama wako? Haki I can feel the pain your woman is going through.. Mtu yupo mkoa mwingine anakuacha unalea mtoto peke yako then hana msaada wowote kwako... Wanawake tuna kazi sana haki ya nani! Ndio maana huyo dada anaona bora hata ukamsaidie kubembeleza mtoto usiku maana thats the best you can do!
 
Mwanaume na wewe kweli wataka kunyenyua kende zako uende ukalelewe mambo ya aibu, endelea kukaza utoboe kwa juhudi zako ueshimiwe sisi wanawake tusimanga hatari tunapotoa.
 
Mwache aende akakune nazi.

Mwambie awe mwanaume aache upuuzi.
 
Mtaji anaofanyia huko aliko aende nao alipo mkewe akafanyie huko au hizo mishe akapigie alipo mkewe ajue heri wawili kuliko mmoja akiwa karibu na wife atapiga hatua zaidi ila asikubali kwenda kukaa tu nyumbani
 
Nenda kakae na familia yako mkuu,

Mtoto analelewa na Baba na mama, tofauti ya hapo unaweza kuwa na mtoto mwenye walakini kitabia na chanzo kikawa wewe kuwa mbali, bila kujua wewe ndio chanzo.

Huna uwezo wa kuhudumia familia na bado familia haipo karibu na wewe sasa hiyo si Dhambi mkuu?

Nikushauli kitu, nenda kaishi na mama watoto wako, pili uwe muwazi na mkweli kwake, umsikilize vizuri kwa kila jambo nahisi ana mpango mzuri juu yako.

Kwa namna yoyote pambana jitume kuhakikisha wallet yako inaongea na usichague kazi. One thing stay focus na familia yako tu usiangalie mtu mwingine.
 
Kama ni mke wake wa ndoa arud haraka wakasaidiane kulea mtoto na inaonyesha mwanamke anampenda kwa hiyo hatashindwa kumpa hata kamtaji kadogo kaa-kuanzia,
Ila pia kama wajafunga ndoa wafunge haraka na wamlee mwanao katika ndoa na wakumbuke ndoa siyo lazima kuwe na sherehe.
 
Na yeye ampe sharti huyo mwanamke amwambie kama unataka nije basi niangalizie mtaji nianze biashara tusaidiane.

Masharti wakati huna mbele wala nyuma.! Aweke mashart aone mtoto wake anavyo pata baba wa kambo asie na mashart faster.
 

MKUU,

UNAMAANISHA KABISA-
WATAKA KWENDA KUMTEGEMEA MWANAMKE???!!!

NAKUPA WIKI 3 TU,
UTAKUJA KUSIMULIA KITAKACHOKUKUTA!!!

Tatizo mnaishi kukalili, mtamfanya mwenzenu hata akiambiwa ukweli aone ananyanyaswa. Cha msingi akajitume maana mafanikio ni kujituma.
 
Kama anakupenda akutafutie kazi ya maaana kama ikishindikana basi endelea zako kupiga debe manake ww ni baba pambna uwezavyo uweze kutunza familia ila kama unakipaji cha kua marioo wala usitake ushauri nenda baba ukaangukie kakitongaa
 
Upo serious kabisa unaomba ushauri kwenye hili?

 
mimi naamini huyo rafiki yako ni wewe mwenyewe, ila chakufanya huwezi kabisa hata kupata milion tatu ukafanya biashara maana kwa maisha ya sasa usiwekeze fikra kwenye kuajiriwa sana. ila huyo baby wako nae anakupenda ndio maana anakuonea huruma
Upo sahihi mkuu tena hata mil3 nyingi.Business zipo kibao tena mtaji wa laki5 tu anaweza ingiza kilasiku sichini ya 20000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…