Tumepoteza Tunu ya kuaminiana (Tunahitaji Kuirudisha)

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
14,470
22,843
Justice must not only be done, but it must also be seen to be done.”

Kuna mambo yamekuwa yakitokea na watu kurushiana shutuma kwamba ni huyu au yule amefanya.., Mbaya zaidi Kuna upande hawana Imani na Wachunguzaji (Vyombo Husika) kwahio Uchunguzi wowote utakaofanyika bado watu hawataridhika kwa kusema huenda fulani amesingiziwa au aliyeshikwa ndiye, sio.

Kwahio sababu Kuaminiana ni Muhimu sana Katika Ustawi wa Jamii ni muhimu tukarudisha imani hiyo hususan kwa taasisi ambazo zinatulinda.

Hivyo binafsi nashauri sababu watu Hawana Imani na pande zote kuhusu uchunguzi wa yanayotokea, ni Vema ikaja Taasisi ya uchunguzi either kutoka nje au iundwe TUME itakayojumuisha pande zote ambazo haziaminiani ili uchunguzi ufanyike na wenye hatia washikwe (no matter wanatokea upande gani Wasioamini au Wasioaminiwa) ili tukate huu mchicha kabla haujakuwa na kuwa Mbuyu sababu tutashindwa kuuhimili. (Hopefully Mchicha huo haujawa Mbuyu Tayari).
 
Waafrika haya masuala ya demokrasia sio jadi yetu. Tulilazimisha tu.
Mfumo wowote ule inabidi uaminiwe na wananchi (its a social contract) sasa kutokuwa na imani na mifumo / taasisi ni hatua moja kabla ya anarchy... tunapoelekea tunapotea ni bora tusimame au turudi nyuma na kutafuta njia...
 
Back
Top Bottom