1. Alianza kuzima bunge live, tukapigapiga kelele tukanyamaza(si wanaharakati wala viongozi wa dini waliobodha kulishughulikia hili, wakaachiwa UKAWA na ACT, matokeo yake likawashinda). J. Kikwete hakuwa mjinga kuruhusu bunge live!
2. Akaja akaikanyaga katiba aliyoapa kuilinda kwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na maandamano. Wanaharakati na viongozi wa dini wakawa kimya! Wanasiasa wamepigapiga kelele pia limewashinda
3. Baada ya hapo zikaja kauli za kibabe kuwatishia watakaojitokeza kuhoji (Atakayeleta fyoko fyoko atanitambua, mimi sijaribiwi,etc) tukamuacha!
4. Akaja na version ya uteuzi wa makada wa CCM kwenye kila nafasi, bila kujali professionalism wala uzoefu, kikubwa uwe kada. Tumepiga kelele tumenyamaza
5. Amesitisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya bila kumshirikisha yoyote. Hakuna hata anayejali hadi najiuliza kama kweli tulikuwa tunaihitaji katiba mpya au ilikuwa ni njia tu ya kumsumbua Kikwete coz tuliaminishwa na baadhi ya makanisa kuwa ni mbaya sana na hafai
6. Sasa Amekuja na mkakati wa kunyamazisha wanaomkosoa, kuanza kupambana na mitandao kama JamiiForums, kupambana na akina Lema na Lissu. Tutapiga kelele tutamwacha aendelee tu(hapa ndo tunaona unafiki wa viongozi wetu wa dini na wanaharakati ambao walikuwa so vocal kipindi cha JK, but awamu hii ni kama wamemwagiwa maji!
My worry ni kwamba Rais Magufuli anaset precedence (atakuwa ndo reference) ya uongozi Tanzania hata kwa viongozi watakaofuatia. Raisi ajaye naye akizuia shughuli za kidemokrasia hatutakuwa na uhalali wala nguvu kumpinga kwa kuwa huyu tumemuachia. Itakuwa ni unafiki wa hali ya juu kwa viongozi wa dini na wanaharakati kumsumbua raisi ajaye kwa kumuachia huyu afanye atakavyo