Tumekosa Mikopo, wahusika wako kimya!

chendelela

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
1,145
1,007
Wakuu,

Naandika uzi huu kwa masikitiko makubwa kwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu tusio wanufaika wa mkopo, hususani wale tunaoendelea kwa mwaka wa 2 na na 3.

Inauma sana iweje baadhi ya wanafunzi wapewe mikopo na wengine tukose ila hali tuna sifa ya kupatiwa mikopo? Shirikisho la vyuo vikuu mko wapi nyie kuwatetea wenzenu ambao tuna hali ngumu na tumetoka katika mazingira magumu na hii inakuwa kikwazo kwetu watoto wa maskini kuendelea na masomo.

Na kitu kibaya zaidi ni manyanyaso tunayoyapata kutoka kwa watawala ktk vyuo hususan UDOM college ya education kwa nini wanakuwa na roho za kishetani pindi mwanafunzi aendapokuwaeleza amekwama kukamilisha ada kwa wakati? Hi haikubaliki hata kidogo tuoneen huruma watoto wa maskini nasi tuweze kusoma na hivyo kuwa msaada kwa jamii zetu.

My take.
Serikali tusaidieni watoto wa maskin nasi tuweze kupatiwa mkopo ili tuweze kuendelea na masomo kwan hyo n haki yetu kwa sababu tuna vigezo vyote after all hatupewi bure tutakatwa baada ya kumaliza masomo.Inauma sana kupokwa haki ya msingi ya kupata elimu.

We have to enjoy our cake of nation regardless our financial status,social status,political affiliation,religious affiliation as well.
 
Last edited by a moderator:
pole sana mkuu,,vumilia tu,,hi ndo kusema alienacho anaongezewa na asiyenacho ata anachozan anacho anapolwa,,hi ndo Tanzania,,mm nipo mwaka wa kwanza lakn sisem uongo najutaaa,,kwan cjawai kuish maisha magum namna hii,ni stor ndef ila pole ndg yang
 
Tena mbaya zaidi kabla ya kuomba tulienda kuomba mwongozo na tukaambiwa prioty itakuwa ni course tena wakatoa na mfano wao wanaoupenda sana akiomba mwanafunz wa udaktari haijalishi amemaliza mwaka 1980 ye atapata tu maana course yake ni tija kwa taifa.. tulipoenda tena hahahahah jamaa watukana kuwa mwaka ndo kigezo cha kwanza... nilitamani kulia pale mwanafunz mwenzangu wa ualimu wa sayansi dodoma first cont alipojibiwa kuwa arudi tu nyumbani maana hapati kitu....
 
 
 
Wameanza kufikiria wanafunzi wa private universities wasipewe mikopo-kwa sauti ya Kitila Mkumbo. Lisemwalo lipo kama halipo laja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…