Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,647
- 119,252
Wanabodi,
Haya ni mapendekezo yangu kwa miswada mitatu ya sheria ya uchaguzi, Sheria ya vyama vya siasa na Tume ya uchaguzi.
Nilipendekeza
1. Sheria yetu ya uchaguzi tunayoitunga, ifuate katiba ya JMT ibara ya 5 na Ibara ya 21.
2. Ibara ya 5 ni Haki ya kila Mtanzania kuwa huru kumchagua kiongozi anayemtaka.
3. Ibara ya 21 ni Haki ya kila Mtanzania kuwa huru kugombea na kuchaguliwa kuwa kiongozi.
4. Tufanye mabadiliko madogo ya katiba kuondoa ubatili kwenye ibara ya 39 na 67, uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu.
5. Turudishe haki za Mtanzania zilizoporwa za kuchagua na kuchaguliwa.
6. Tume ya uchaguzi iitwe Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi
7. Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ufanyike siku moja.
8. Chaguzi zote mbili zisimamiwe na Tume moja Huru na Shirikishi ya Uchaguzi.
9. Uongozi wa vyama vya siasa, sio ajira!, ni uongozi wa kujitolea, viongozi wa vyama vya siasa hawapaswi kulipwa mishahara, ni posho tuu!.
10. Tuifute ruzuku kwa Vyama vya Siasa na badala yake tutoe ruzuku kwa yatima, wajane, wazee, wasiojoweza na wenye ulemavu.
Leo serikali imetoa taarifa ya kukubalika rasmi pendekezo moja
Japo mapendekezo yangu mengine yote yamekataliwa, ukiomba mambo 10, mambo 9 yakakataliwa, jambo moja likakubaliwa, hatua ya kwanza ni kushukuru na kupongeza kwa hilo moja lililokubaliwa, halafu uendelee kupigania yale 9 yaliyobakia yaliyo kataliwa.
Pongezi serikali yetu sikivu kubadili jina la Tume ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Uchaguzi. Naomba sana lisiwe ni jina tuu, lakini mambo yakawa ni yale yale!, sote tumeshuhudia kilichotokea Zanzibar ile 2015, ZEC ni Tume huru na Shirikishi lakini kilichotokea... Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
Hivyo naipongeza sana serikali yetu sikivu kukubali kubadili jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, kuwa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, swali kama Itakuwa Huru Kweli au ni Jina Tuu bado lipo mpaka tuushuhudie huo uhuru!. Ukiomba Mambo 10 Ukapewa 1, Shukuru kwa Hilo 1. Asante sana serikali yetu kwa INEC!. Yale 9 yaliyobakia, kazi inaendelea na ikibidi, kuna watu watabisha hodi mahakamani!.
Nimalizie kwa kuendelea kusisitiza Watanzania tuwe ni watu wa shukrani, tushukuru kwa madogo ili tuweze kujaaliwa makubwa!.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Rejea za Mwandishi Kuhusu Sheria Hizi.

- Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
- Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
- Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi: Je Tupige Ndege Wawili kwa Jiwe Moja kwa Uchaguzi Serikali za Mitaa/Mkuu, Ufanyike Siku Moja au Tuendeleze Mazoea?
- Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana!
- Licha ya Mapungufu, Sheria Mpya ya Uchaguzi Pia ina Mazuri Yake!, Imerejesha Mamlaka ya Uchaguzi kwa Wananchi, Hakuna Kupita Bila Kupingwa!.
- Asante Rais Samia kwa Muswada huu. Umuhimu wa mabadiliko ya Katiba kabla ya Sheria hii bado ni muhimu sana. Huu ni uchambuzi Wangu - Part 1
- Je, wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni batili? Ni mvinyo wa zamani, kwenye chupa mpya? Why ubatili huu?
- Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!
- Tujifunze kuwa na Shukrani kwa Madogo ili Tupatiwe Makubwa!. Japo Tulitaka Kikubwa, Tumepewa Kiduchu!, Tukipokee Tushukuru, au Tususe Kudai Kikubwa?.
- Lile fupa lililowashinda marais wanaume 4, rais mwanamke 1 aligegeda kama mlenda!. Miswada 3 ya ukombozi mpya wa taifa letu yatua bungeni asubuhi hii
- Ombi kwa Rais Samia: Japo wengi wape, wachache pia wasikilizwe, Hoja ya kufanya minimum reforms za Katiba ni hoja ya msingi sana kuliko hata Sheria!.
- Haki, Haki, Haki! Serikali, Bunge na Mahakama hazina uwezo wala mamlaka ya kupora haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Je, jicho ona litaliona hili?
- Rais Samia Japo Si Mwanasheria, Lakini Anaijua Katiba ni Sheria Mama Yenye Haki Zote Ndani ya JMT. Je Aruhusu Haki Hizi Ziporwe Tena? Au, Azirejeshe?
- Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa! Sheria ya Uchaguzi ni kosa. Kwanini tunarudia kosa? Haki si hisani, ni stahiki. Bunge tutendeeni haki!
- Je, Siasa ni Ajira? Ni Kazi ya Mshahara au ni Kazi ya Kujitolea? Kwa Umasikini Wetu Huu Uliotopea, Ni Haki Kulipa Ruzuku kwa Vyama vya Siasa?
- Maoni yangu kwenye Mkutano wa Vyama vya Siasa kuhusu Muswada wa Sheria Mpya ya Uchaguzi. Muswada sio batilifu, ni Muswada batili
- Tuombe Mwaka 2024 Uwe ni Mwaka wa Mageuzi ya Kweli ya Kidemokrasia ya Kweli Tanzania. Tume Huru, Uchaguzi Huru na wa Haki! Happy New Year!
- Shurti la Mgombea Kudhaminiwa na Chama cha Siasa ni Shurti Batili, Lililochomekewa Kiubatili Ndani ya Katiba Yetu. Kwanini Tunalikumbatia?
- KMT Wiki Hii Msajili wa Vyama, Jaji Mutungi, Father Kitima, Balozi Amina Salum Ali, Ismail Jussa, Mjengwa, Selasini, Kibamba, Cheyo Waunguruma!.