Tume Huru ya Uchaguzi Iliyokosa Uhuru

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
18,970
47,843
Uhuni, usanii, ghiliba, ulaghai na hadaa ya Serikali ya CCM na Rais Samia kuhusiana na Tume ya Uchaguzi kwa Watanzania, inadhihirisha dhamira yao mbaya kwa Taifa letu.

Serikali ya CCM inatumia kila mbinu na hadaa kuhakikisha nchi kamwe haiwi na Tume Huru ya Uchaguzi, wala uchaguzi huru na wa haki, wala katiba nzuri mpya.

Wanakuja na hadaa za kila namna wakiamini kuwa wananchi hawana akili ya kutambua dhamira zao chafu.

Baadhi ya hadaa na hila:

Rais Samia alipochukua tu madaraka alisema kuwa wanaodai katiba watulie, kwa sababu anajenga uchumi kwanza. Hii ilikuwa ni hadaa kubwa inayodhihirisha Rais Samia hana dhamira kabisa ya kuiona nchi inaoongozwa na katiba nzuri mpya. Suala la ujenzi wa uchumi halina mwisho. Hivyo hakuma muda utakaosema kuwa sasa nimemaliza kujenga uchumi. Kauli yake ile ilimaanisha kuwa hataki katiba mpya. Kulidhihirisha hilo, walimkamata Mbowe na kumbambikia kosa la ughaidi kwa sababu tu alikuwa akiongoza harakati za kudai katiba mpya wakati huo.

Wakati kazi kubwa ya kitaalam na shirikishi, ya mchakato wa katiba mpya ilifanywa na Tume ya Jaji Warioba, Samia katika kuhakikisha dhamira yake isiyo njema, aliamua kuunda kamati yake bandia ya katiba mpya ambayo haitambuliwi na sheria yoyote ili kuwahadaa wenye uelewa mdogo waone kama vile kuna hatua zinapigwa.

Hata hiyo tume bandia ilipomaliza kazi yake, kwa kupitia waziri wake Ndumbaro akaja na hadaa nyingine kuwa Watanzania wanatakiwa kufundishwa kuhusu katiba mpya kwa miaka mitatu!!

Baadaye alipoona kuwa amefanikiwa katika hadaa, akaona awe muwazi. Akatamka wazi kuwa katiba si chochote ni kijitabu tu. Hapo alihitimisha na kupeleka ujumbe kwa Watanzania kuwa yote ya huko nyuma aliyokuwa akiyasema ilikuwa hadaa.

Baada ya kupata mafanikio kwenye hadaa ya katiba, akahamia kwenye hadaa ya Tume ya Uchaguzi, nako anaamini lazima atafanikiwa, kwa vile anaamini Watanzania ni wajinga wasioweza kutambua hadaa.

Kwenye hesabu, tunasema kuwa:

Kama a = x, na x = c; basi a = c.

Kama majina ya viongozi wa Tume ya Rais yanapendekezwa na Wajumbe wa kamati ya usaili, na wajumbe wa kamati ya usaili ni wateuliwa wa Rais, ni sawa na kusema kuwa Rais ndiye anapendekeza majina ya viongozi wa Tume ya Uchaguzi, na yeye mwenyewe tena ndiye anayewateua na kuwathibitisha kuwa viongozi wa Tume ya uchaguzi. Na kwenye hadaa hii, Samia anaona pia amefanikiwa kuwadanganya Watanzania waamini kuwa sasa Tanzania ina Tume Huru ya Uchaguzi kwa kubadilisha tu jina lake.

Wito:
Watanzania wote tushikamane kuukemea udikteta huu, kuukataa ulaghai huu, hata kama tukipuuzwa, tuendelee kupiga kelele Duniani kote, hata kama hakuna kitakachobadilika, lakini Duniani nzima itambue kuwa Tanzania hatujawahi kuwa na Tume huru ya uchaguzi, hatujawahi kuwa na uchaguzi huru na wa haki wala hatujawahi kuwa na demokrasia ya kweli, bali kinachobadilika huwa ni kiwango tu cha udikteta kwa kutegemea Rais wa wakati huu ni dikteta kamili, dikteta uchwara, dikteta hadaa au dikteta wa kuuma na kupuliza.

Mbowe na wenzako msitegemee kushuhudia uchaguzi halisi wa wananchi katika chaguzi zijazo. Tusijifanye vipofu wa kuona yanayoendelea halafu tuje tujifanye tunashtuliwa na matukio ya udikteta wakati wa uchaguzi. Wakati wa kupinga udikteta kwenye uchaguzi ni sasa kuliko kusubiria baada ya matokeo.
 
Mama kaona mnataka katiba mpya ili mpate tume huru, kaona isiwe shida kawaletea.!!
Ila katiba ndio tusahau
 
Back
Top Bottom