Tumalizane na miradi ya umeme iliyopo kabla ya kupokea mikopo ya umeme wa jua

nuporo

JF-Expert Member
Oct 18, 2018
1,534
3,378
Tupo katika harakati za kutegemea umeme unaozalishwa na maji na gesi bado tena tunapokea mikopo ya umeme wa jua hii ina maana gani?

Nimefikiria sana sawa ni vyema kuwa na kutumia nishati aina mbalimbali.

Lakini kwanini tusingejikita kukamilisha miradi ilioanzishwa (Bwawa la Nyerere na gesi) imalizike ambayo itatoa umeme wa uhakika mpaka tuanze kukopa tena mikopo ya umeme wa jua?

Hii imekaaje wajuvi?
 
Kuna mkopo unakuja wa umeme wa upepo.
Gesi tuliaminishwa kuwa tatizo la umeme nchini.

Nchi hii acha tu
 
Sijui kwanini tuna mzaha katika mambo ya muhimu. Yaani unakuta wakati wa kupigia debe mradi maneno kama "tatizo hili litakuwa historia". Kabla hata mradi hujakamilika tayari tumeshaanza mchakato wa mradi mwingine. Matokeo yake ni upotevu wa fedha kwenye miradi ya zamani ambayo hata haijakamilika!!

Kama sio kukosa maarifa katika mipango yetu, basi hila ndio sababu kuu ya kupendekezwa na kutekelezwa kwa miradi hii.
 
ukitaka kucheka nenda uwaulize hao viongozi wezi wa kura, kwanini sio umeme wa gas bali wa maji Utashangaa maelezo yao. Waliosifia umeme wa gas kwa kusema matatizo ya umeme wa maji ni mabadiliko ya tabia nchi, ndio hao hao wanaosifia wa maji sasa. Yaani kimsingi kuna tatizo kubwa kuliko tunavyodhania.
 
Sasa watu wenyewe ndio akina musukuma unategemea nini?
 
Sijui kwanini tuna mzaha katika mambo ya muhimu. Yaani unakuta wakati wa kupigia debe mradi maneno kama "tatizo hili litakuwa historia". Kabla hata mradi hujakamilika tayari tumeshaanza mchakato wa mradi mwingine. Matokeo yake ni upotevu wa fedha kwenye miradi ya zamani ambayo hata haijakamilika!!

Kama sio kukosa maarifa katika mipango yetu, basi hila ndio sababu kuu ya kupendekezwa na kutekelezwa kwa miradi hii.

Na hilo la kukosa maarifa katika mipango yetu, haliko kwenye umeme tu. Bali ni mambo mengi tu. Utoke kwenye elimu, afya, kilimo nk.
 
Tupo katika harakati za kutegemea umeme unaozalishwa na maji na gesi bado tena tunapokea mikopo ya umeme wa jua hii ina maana gani?
Wasipofanya hivyo viongozi waliopo watapata wapi 10%??

Kila mwanasiasa anapambania tumbo lqke.
 
Na hilo la kukosa maarifa katika mipango yetu, haliko kwenye umeme tu. Bali ni mambo mengi tu. Utoke kwenye elimu, afya, kilimo nk.
Unaweza kuona Kilimo Kwanza ilivoanza na kuisha huku takwimu zikionesha au mgando au kusinyaa kwa sekta hiyo. Tukaja "Uchumi wa viwanda" ambao kimsingi ulipaswa kuwa ni mwitikio wa bidhaa za mazao kuongezeka. Matokeo yake hata viwanda vimekuwa na tafsiri sio ya kimtaji bali au uzalishaji "idadi ya wanaoajiriwa" (kumbuka kufikia kusema cherehani nne ni kiwanda). Sasa tuko kwenye "Miradi ya kimkakati" na inaelekea ndio jambo kuu sasa.

Incompetence everywhere!!! Kila mkuu wa mkoa na wilaya na waziri ni kutoa tu maagizo. Matokeo yake mambo mengi kufanywa tofauti sehemu tofauti za nchi, kutaka mambo tusiyokuwa na uwezo nayo katik kupanga kutekeleza na hata kuratibu na kudhibiti. Mwisho wa siku tunabaki kuwa wajuzi wa mambo kifikra tu. Inaumiza.
 
Back
Top Bottom