Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,032
- 4,735
Natoka Mwanza, kutoka Kibaha hadi Kimara nimeona tayari vituo zaidi ya Nane vya Mafuta vimejengwa kwenye hifadhi ya barabara.
Ninaamini hivi vituo havikuwepo kwenye ramani ya barabara kwa wingi huu. Lakini pia naamini haya maeneo hayakutengwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta lakini kwa sababu ya rushwa kila mtu amemega eneo lake anajenga anavyojisikia.
Kwa namna hii miaka siyo mingi foleni itakuwa kubwa sana kwa sababu magari yatakuwa yanaingia kwenye vituo vya mafuta na kutoka hivyo kupelekea speed tarajiwa kupungua barabarani.
Lakini pia vituo hivi vinaonekana vimeanza kutumika kupaki malori makubwa huku baadhi ya malori kutoka bandarini yakija kujaza mafuta nakupanga foleni barabarani katikati.
Mimi ninayekuja mara moja moja huku tayari nimeona huu uhalifu ,je wananchi wa DAR mnafurahia haya?
Lakini pia tunazungumzia kupanga miji, hakuna mji wowote uliopangwa Duniani wenye utitiri wa petrol station Duniani. Sisi tunashindwa nini kuiga wenzetu walivyofanikiwa?
Mwisho, hivi vituo kwa majina tu inaleta picha kwamba wapo watumishi wa umma wanapiga fedha serikalini na kuja kuzielekeza kwenye biashara ya mafuta. Hakuna wafanyabiashara wenye business plan watatega vituo vya mafuta kama inavyofanyika sasa.
Labda TANROADS watueleze kama haya wanayofanya ndiyo yaliyopelekea kuwavunjia watu nyumba na biashara zao bila fidia wakati wa JPM? Kwanini tunatumia madaraka yetu kuharibu kesho ya watoto na wajukuu wetu? Nini tathimini ya kimazingira kwenye mji wenye watu wengi kama huu kujaza vituo vya mafuta?
Kwanini kama tulitaka kuwekeza tusingeweka vituo vya gesi?