Tukiwa madarakani ni muhimu kusoma vitabu hivi

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,255
1,562
Kwenye maisha tunayoishi, ni muhimu kujifunza kupitia vitabu hivi,

1. THINGS FALL APART - By Sabaya
Itakusaidia saana kujua kuwa kuna siku madaraka huisha na kutakiwa kuwajibika kwa yale uliyoyatenda iwe Mbinguni au hapa duniani, kitabu hiki kitufundishe kuwa ikifika nyakati hizi ni Muhimu kumrudia Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wa kutusamehe .

2. NO LONGER AT EASE- By Makonda
Itakusaidia kujua mambo huwa yanaisha, ufalme huwa unapita, nyakati husogea, mambo hubadilika na Watu wapya huja, uliyatenda kwa sababu uliaminiwa na sasa wameaminiwa wengine, lakini tutalipwa kwa yale tuliyoyatenda wakati tumeaminiwa. Tulio watendea wema watatuombea daima na tulio watendea ubaya watatulilia daima.

3. THE RIVER BETWEEN - By Balozi Slow
Hiki kitabu kitakuchanganya maana kuna nyakati huelewi ukae upande gani kama yule mzee....Ila ni muhimu kuchagua upande ulio sahihi na kuamini yaliyopita hayawezi jirudia tena. Amini kuwa yamepita,yamekwisha usiendelee kuishi kwende ndoto umeaminiwa tena piga kazi.

Tuendelee Kumuombea Mama yetu Kipenzi, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayofanya, Tanzania si kijiji tena.

Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania, Mbariki Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 
hahaaaaaaaaaaaaaaa!
Umenikumbusha mbali sana enzi za "skonga'
Lakini binadamu tunatakiwa kujua kuna leo na kesho.
Sabaya na wenzake hawakuona hilo, waliona nchi ni yao na itakuwa hivyo milele.
😄
 
Hao wote wakiupata ujumbe wako huko walipowanang'ata vidole almanusura vikatike kwa meno 😂
 
Back
Top Bottom