Tukisema ligi ya EPL ndo kipimo Sahihi kwa Makocha na Wachezaji Tutakosea?

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Binafsi sina budi kusema ligi ya Uingereza ndio kipimo sahihi cha wachezaji na Makocha duniani ni kama vile mitihani ya Darasa la 4 au form 2 ukiweza kufaulu basi umeingia darasa lingine ukifeli kurudia kunakuhusu.

Wamekuja Wachezaji wengi wakiwa bora kabisa kutoka ligi walizotoka ila wamefika pale UINGEREZA wamechemka vibaya sana kwa uchache wao kama vile ROBIHNO,MATEJA KEZMAN,SHEVCHENKO,JO,FALCAO,DI MARIA,PAULIHNO...NK

Na pia kwa sasa tunashuhudia kocha bora kabsa GUARDIOLA akilambishwa sakafu na baadhi ya timu za kawaida kabisa pale Uingereza ambapo kwa ligi alizotoka BUNDESLIGA NA LA LIGA msimu kama huu tiyari angekua ameshatangaza Ubingwa au kumwacha mpinzani wake kwa tofauti ya pointi kubwa sana ila kwa sasa mambo ni kinyume.

JE VIGEZO HIVYO NI HALALI KUSEMA LIGI YA UINGEREZA NI KIPIMO SAHIHI CHA MAKOCHA NA WACHEZAJI?
 
unazungumziaje wachezaji wa uingereza ambao wameshindwa kuprove kwenye ligi nyingine?

unazungumziaje timu za
uingereza kushindwa kuprove kwenye ligi ya mabingwa na europa.sevilla kila siku anachukua yeye na uefa madrid na barca wanapokezana kila siku kwanini timu za uingereza zinashondwa kuleta changamoto kama ni bora?
huwezi kuchukua kocha mmoja ambaye hajamaliza hata msimu mmoja ndiyo iwe kipimo chako.
 
Mimi nadhani kinachowashinda timu nyingi za EPL kwenye UCL ni fixture zao. Fixture za EPL ni ngumu sana na hamna kupumzika kama ligi nyingine, so mda mwingi wachezaji wanachoka lakini epl ni the best aisee.

Hao spain au german wangekua na fixture ngumu kama epl wangeshidwa tu.
 
hapa nimezungumzia Makocha na wachezaji sijataja ubora wa timu moja moja.

David berkam alitoka Man utd akaenda R.madrid bado akafanya vizuri,sawa sawa na Christian Ronaldo na pia Samir Nasri kuna Nzozi wote wanafanya Vizuri
 
Unamzungumziaje Zlatan mliokuwa mkimbeza alipokuwa La liga, Serie A na Ligue 1 kwamba yupo ligi dhaifu, lakini ona anavyowapa shida mabeki wa EPL. Unazungumziaje wachezaji kama Sanchez na Ozil, walivyokuwa wakikalia bench kile la liga na sasa ndo mastaa hapo EPL. Kinachomuangusha Pep ni wachezaji alionao, umri umeenda sana lakini sio kocha dhaifu hata kidogo.
 
kuhusu kukalia benchi sio sababu kwamba mchezaji ni mbovu kuna vigezo vingi kama vile mfumo wa kocha Ozil ametoka real madrid akiwa ni mchezaji mzuri tu na pia Sanchez mfumo wa Barcelona ulimkataa ila sio kwamba alikua mbovu
 
hapa nimezungumzia Makocha na wachezaji sijataja ubora wa timu moja moja.

David berkam alitoka Man utd akaenda R.madrid bado akafanya vizuri,sawa sawa na Christian Ronaldo na pia Samir Nasri kuna Nzozi wote wanafanya Vizuri
sasa mkuu ligi inajengwa na nini timu au matofali?
 
timu za uingereza huwa hazina time na europa,ndomana timu kama spurs huweka kikosi dhaifu kwenye europa,sevila ndo malengo yake hayo,hana kombe lingne analoota
 
kuhusu kukalia benchi sio sababu kwamba mchezaji ni mbovu kuna vigezo vingi kama vile mfumo wa kocha Ozil ametoka real madrid akiwa ni mchezaji mzuri tu na pia Sanchez mfumo wa Barcelona ulimkataa ila sio kwamba alikua mbovu
Ndo hapo sasa ujue kocha au mchezaji kufeli ligi moja na kufaulu ligi nyingine sio kwamba ni dhaifu, usiwe na double standard mkuu. Ujue hapo kuna mambo mengi yamechangia pia kwa Pep kufanya vibaya EPL ikiwepo suala la wachezaji kutokumasta vizur mfumo mpya wa kocha(tik tak) style.
 
timu za uingereza huwa hazina time na europa,ndomana timu kama spurs huweka kikosi dhaifu kwenye europa,sevila ndo malengo yake hayo,hana kombe lingne analoota
Acha kujifariji mkuu, liverpool msimu uliopita mbona aliutolea macho bahati mbaya akala kichapo cha maana. Hiyo Spurs msimu huu mbona imeshindwa kwenda kwenye 16 bora UCL kama haitaki europa alafu ikiwa kwenye kundi lenye timu dhaifu kama yenyewe.
 
Duh hili swali lako pumba kabisa.hata mule mule ndani tu wachezaji wa kiingereza wanafunikwa na wageni.hapo ishu ni ligi ya uingereza siyo wachezaji wa kiingereza
 
Acha kujifariji mkuu, liverpool msimu uliopita mbona aliutolea macho bahati mbaya akala kichapo cha maana. Hiyo Spurs msimu huu mbona imeshindwa kwenda kwenye 16 bora UCL kama haitaki europa alafu ikiwa kwenye kundi lenye timu dhaifu kama yenyewe.
umeona liver tu..tena kwa mwaka jana!..ikiwa na mwalim mpya,alietaka kwenda uefa kwa mgongo wa euro,spurs ktoka makundi sio tatizo,ila lengo lake ubingwa wa epl
 
Hakuna cha ubovu ni mifumo,hata moses mifumo ya chelsea ilmkataa lakini alvyokuja conte anashine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…