Doto12
JF-Expert Member
- Nov 2, 2023
- 613
- 1,103
Habari zenu wana JF
Niliwahi kuandika juu ya suala ya usafirishaji kwenye majiji yetu yote. Nilikwenda mbali zaidi kwamba inafika wakati sio bisahara tena bali ni huduma.
Serikali yetu inazorotesha maendeleo ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla kwa kung'ang'ania hizi daladala zinazosababisha matatizo lukuki kwenye majiji ya nchi maskini duniani.
Baadhi ya matatizo yanayosababishwa na daladala hapa nchini maeneo ya majiji yetu hususana jiji la dar es salaam ni haya:-
1. Kupoteza muda. Muda mwingi sana unapotea barabarani na msababishaji mkubwa ni hizi daladala zinazosimama kila konda na dereva wake wanapoona wanahaja bila sababu husimama kuitia abiria. Ikumbukwe Dsm sio mtaa tena ni jiji lenye shughuli nyingi.
2. Daladala nyingi chakavu, na hii ninsababu ya kupoteza muda. Na kwamba hizi sababu zote ndizo askari wetu huchukulia nafasi kupokea rushwa.
3. Dar es salaam haihitaji daladala za kibiashara bali mabasi ya kutoa huduma ya usafirishaji, daladala ni lazima zitoke nje kabisa ya mji ya sio nje tu. Nje ya mkoa mzima na kuwepo kampuni..hii iliongelewa lkn daladala na wamiliki wao waliizidi nguvu serikali(sina ushahidi) hii mijadala yetu wenyewe kwamba bahersa alikuwa alete mabasi kwa maelefu atoe huduma ya usafirishaji jijini.
4. Kama kuna kitu watu hawakijui ni wamiliki wa daladala jijini dsm hawa ni wakali sana sana inapotekea maslahi ya kufanya biashara ya daladala jijini. Lkn je wako wapi baada ya fedheha hii ya rushwa waziwazi. Nani hajui magari dsm yanatoa rushwa sana jijini.(hapa ole wangu) lkn teyar video imeonyesha wazi hakuna siri tena. Wamiliki hawa ndio source kubwa ya daladala kusumbua jijini na majiji mengi.
5. Serikali yoyote duniani inalinda maslah za wengi, wenye daladala hawa watu ni wengi mno, ukigusa hapa kuziondoa ili yabaki mabasi ya mwendokasi na makampuni ya kutoa huduma. Ilifikia wkt hata yale mawazo ya kujiunga kila kampuni yenye mabasi 100 ndio wajisajiri na mabasi yawe makubwa ikashindikana.
Ushauri.
Ili tusiwe kama India(New Delhi), Lagos misongamano ya kuua mtu tuachane na kuooneana kama nchi nyingi zinazoendelea kwamba haya ndio maisha lazima daladala ziende nje ya majiji na kampuni zifanye kazi badala yake.
Barabara kuu hizi daladala zitoke. Zikafanyie pembeni kabisa. Kwa mfano dar es salaam zitoke zifanyie pwani na morogoro. Mbeya daladala zitoke nje, mwanza hivyo hivyo, Arusha, Tanga na Moshi. Bado nchi ni kubwa na ina watu. Mji kama Geita, kampuni zifanye kazi sio daladala nk nk
Kinachosababisha hili lisifanyike(visingizio)
1. Ajira kwa madereva na makonda
2. Watu wanapata chochote
3. Wamiliki kuwa nyuma ya pazia na hawa ji watu na ajira zao mbadala. Hizi ni vitega uchumi vyao.
Suluhisho.
Kuachana na mawazo haya yanayodidimiza uchumi wa mtu mmoja mmoja kisa vijisababu vya ajira na kubebana.
Kufikiria mbali zaidi kwamba bado hizi daladala zitafanya vizuri tu nje na majiji.