mbunge wetu mtarajiwa kwa jimbo la segerea 2020,anena haya katika ukurasa wake wa FB.
••••••••••••••
Tumesema mara nyingi kwamba
kitu kinachoharibia utawala wa
awamu ya tano ni kutoacha
masuala ya nchi yaendeshwe kwa
mifumo iliyowekwa kikatiba na
kisheria. Badala yake maamuzi
mengi yanafanywa kwa matakwa
ya viongozi. Hii imeleta na
itaendelea kuleta migongano
mingi ya mihimili na mamlaka za
nchi, na kuwachanganya
wananchi.
Jana hadi leo Polisi na BASATA
waliona kwamba wimbo wa WAPO
ulioimbwa na msanii Nay Wa
Mitego hauna maadili na msanii
huyo akakamatwa na kuwekwa
ndani na wimbo huo kufungiwa.
Baadaye leo Rais akaamua
kwamba wimbo huo hauna tatizo
la kimaadili na hivyo uendelee tu
kupigwa.
Hii ni moja ya mifano ya
kutofuatwa kwa mifumo ya
kiutawala hapa nchini. Kwa mfano
katika jambo hili wananchi
wanajiuliza nani mwenye mamlaka
ya kuamua ni wimbo upi una
maadili na upi hauna. Je, ni Rais
au Polisi au BASATA?
Wimbo wa Nay Wa Mitego wa
WAPO umeruhusiwa na Rais, je,
nyimbo zingine zitakazopigwa
kuanzia sasa hata kama Polisi na
BASATA wataona hazina maadili,
itabidi waende Ikulu kwanza
kumchezea Rais na yeye ndiye
aamue? Ni vizuri tukajua.