Tujadili: Muundo wa bendi za muziki wa dansi

Septem

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
313
404
Wadau wa muziki pendwa wa dansi(rhumba na soukous) kutoka tanzania na kongo nina waarika tujadili juu ya Muundo, uongozi na umiliki wa band mbalimbali. Hapa nitatoa ufahamu wangu juu ya Muundo wa band kadhaa hasa za kongo.

Kongo kwa sasa kuna band kadhaa kubwa lakini vinara hasa bado zinashikiriwa na kizazi cha nne i.e Wenge Maison Mere-WMM yake Ngiama werason, Quarter latin int'-QL yake Koffi olomide, Wenge bcbg yake mpiana. Zipo band zilikua bora za miaka ya 2000 mwanzoni. Mf Les marquis de maison mere yao wakali wa sauti jack mulopwe na padre ferre golla na mkali wa Atalakus bill kalundji a.k.a bill clinton. Kwa ujumla ufuatao ni Muundo wa band hz za dansi. Nitakua nachukua mifano tofauti(tz&congo).

KIONGOZI WA BENDI.
Hapa inategemea hasa na umiliki. Mfano bendi ikiwa inamilikiwa na mtu asiyemuimbaji, chukua mfano wa AKUDO(kifupi cha majina Athumani, Kulwa na Doto-watoto mh kapuya-ambaye ndie mmiliki hasa), kiongozi huyu anakua tu ni kama kiungo kati ya wamiliki na wanamuziki. So anakua na supervisory role lakini hana sauti ya mwisho. Mfano Fm Academia kiongozi wa band ni Rais Patcho mwamba (zamani ni nyoshi el saadat). Katika mfumo huu hata kiongozi wa band akiondoka, bendi haiteteleki sana.

Katika mfumo mwingine ambayo mmiliki pia ni muimbaji, huyu ndio kiongozi wa bendi. Yeye ndio msimamizi wa masuala yote mf ya kifedha na kisheria. Mf ni koffi ndan ya QL au werason ndani ya WMM. Mfumo huu kiongozi akiondoka basi huja band nayo ikafa. Chukulia koffi hayupo je QL itasurvive? Nadhani hii ni moja ya sbb ya jahazi taarab kufa baada ya mzee kujitoa.- 'alikua kila kitu'.

2. UTAWALA
band yenye mfumo wa kiongozi wa bendi, mara nyingi kunakua na marafiki au kakikundi ka watu wakaribu wa kiongoz wa band. Hawa kazi yao kumshauri kiongozi juu utendaji na mwenendo wa bendi, kumuunganisha na deals mbalimbali. Lakini katika mfumo wa kwanza wa bendi, watawala wanakua ni waajiriwa rasmi katika vitengo mbalimbali mfn, msemaji, mtu wa fedha, hr. Hawa ndio wanafanya shughuli zote za kiundeshaji bendi. Bendi kama twanga, Management ya ASET Company ndio Utawala. Katika bendi kama wenge au ql, hawa ndio custodians wa baadh ya vitu vya bendi members, mfn pasport za wasanii wanakaa nazo. Hii ni sababu ya kuhofia kukimbiwa na wanamuziki.

3. 'NAHODHA WA BENDI'
sina hakika kama ni lugha sahihi nikiita hvyo, ila wakongo wanaita CHEF D'ORCHESTRE. Huyu ni mwanamuziki mkongwe katika bendi na mwenye kipaji kikubwa kiasi cha kung'aa kumfikia kiongozi wa bendi. Majukumu yake hasa ni kuwa kiungo kati ya kiongozi wa bendi na members wengne. Bahati mbaya sana hawa huwa wanajisahau na kuvimba vichwa na kupelekea wasanii wenzao kuhama band, duru za musik congo zinaeleza hii ni moja ya sbb kuu ya migogoro katika bendi.

4. MBADALA WA KIONGOZI
wafaransa wanaita enfant cherie, huyu ni kama mrithi wa kiongozi wa bendi. Anaaminiwa na kusikilizwa. Anakabidhiwa majukumu na kiongozi pindi hayupo. Mf ni boura mpela katika bendi ya QL. Huyu koffi anamchukulia kama ni mwanaye. Au ilivyo heritier watanabe kwa werason kwa sasa, na bill clinton kabla ya 2004. Bendi za tanzania ikoje?

5. MAPEDEJZEE.
Huwezi sikiliza nyimbo za bella, fm academia, twanga usisikie majina kama ndama mtoto wa ngombe, chief kiumbe, apocalyse bella, au kiluvya. Hawa ni wafadhili na ndio wanaochangia kiasi cha fedha kwenye mabendi. Hvyo wanayo sauti na ushawishi.

6. WAIMBAJI
Hii ni safu ya waimbaji katika bendi. Mfn fm academia walikua na safu kali sana, pablo masai, king blaise, 33, patcho, jose mara, jesus katumbi, roger muzungu. Nzimbu n.k

7. RAPA.
Kikongo wanaita atalakus, au animatuer kifaransa, animator kwa kiingereza. Hawa ni wale wanaoimba sehem ya sebene kwenye nyimbo. Ukisikia vipande kama vile utamu wa vanila ee utamu, hawa ndio atalakus. Mf ni chitokololo. Au kina bill clinton wa WMM au kirikou wa koffi.. Pia siku hz wanaimba nyimbo yote-ikiitwa generique- mf nyataquance ya koffi amerap almost yote kirikou.
8. WAPIGA VYOMBO.
Hapa ndio kuna wapiga drums, vinanda na gitaa zote. Hawa ni roho ya bendi.

Huo ni utafiti wangu kutokana na uzoefu mdogo, na maandiko mbalimbali. Nakaribisha nyama zaidi kutoka kwa wadau.
 
Uzi mzuri natamani kumuona hapa kaka yangu GENTAMYCINE

Sijajua nijadili nini katika huu uzi wake Mletaji kwani sijaona Kipya sana sana naona maneno mengi mengi ambayo ni kama vile ameyatoa tu mahala na kaja kuyatupa hapa. Tafadhali sana Dada yangu siku nyingine usirudie tena kuniita katika threads zisizoeleweka kwani ni kama vile unanidhalilisha. Bahati yako tu ni kwamba ninakupenda kunakotukuka mwaaaaahhhhhhhh......
 
Ahahah jaman basi anzisha thread ya uchawi wa wanamuziki wa congo akianzia Pepe kale, werrason, jb na wengineo nakumbuka mda kidogo nipo guest jf nilipita jukwaa hili nikakuta umemquote mtu unamuelezea ndio kisa cha kuwa mfuasi wako na kukupenda nilianzia hapo mwaaaaaaaah too
 
Ringa Dada yaani nakupenda kuliko hata unavyopendwa na uliyenae au na hao wengine. Na ukiona hadi GENTAMYCINE anakupenda jua nimeshakuthibitisha kwa Vigezo vyangu vyote vya Kiumakini hadi kujiridhisha. Vipi unajisikiaje leo kujua au kusikia kutoka Kwangu kabisa kuwa nakupenda?

Hatimaye leo nimejibu rasmi swali langu ambalo nililiuliza katika uzi fulani hivi wiki hii. Anza kujiita tu Mrs. GENTAMYCINE mwaaaaaahhhhhhhhhh......pokea busu langu tafadhali. Yaani natamani tu ningekuwa karibu nawe ili nikupige mabusu ya maana huku nikikutomasatomasa / nikikupetipeti huku na kule hadi tuione dunia hii yote ni yetu wakati kumbe ukweli ni ya Mungu pekee.
 
uwiiiiiiiiiii asante sana nakupenda pia usisahau kuweka hiyo thread basi
 
uwiiiiiiiiiii asante sana nakupenda pia usisahau kuweka hiyo thread basi

Hilo tu Mpenzi wangu mbona Kwangu siyo tatizo. Subiria sasa hivi nashusha kitu na JamiiForums yote sasa itawaka moto ambapo najua kuna watakaonuna na kufurahi pia. Nahamisha akili za Members sasa hivi. I love you Shunie mwaaaahhhhhh....
 
Sijajua nijadili nini katika huu uzi wake Mletaji kwani sijaona Kipya sana sana naona maneno mengi mengi ambayo ni kama vile ameyatoa tu mahala na kaja kuyatupa hapa. Tafadhali sana Dada yangu siku nyingine usirudie tena kuniita katika threads zisizoeleweka kwani ni kama vile unanidhalilisha. Bahati yako tu ni kwamba ninakupenda kunakotukuka mwaaaaahhhhhhhh......
cha maana kipo mkuu, umefunguka kwa shunie kupitia uzi huu
 
Nmeumia sana Hawa Magwiji hawajatajwa
94fbfae8b8ebc457fc3e4daac74d4246.jpg
 
Back
Top Bottom